Sunday, August 25

TUGEUZE CHANGAMOTO KUWA FURSA

0


METHALI – PROVERB

=================

KIHA (Tanzania tribe / Kabila ya Tanzania)

” Akereye inkebhe, mdangi amar irobhe “

ENGLISH (United Kingdom)

” A little of what you fancy does good “

KISWAHILI (Tanzania)

” Kipendacho moyo ni dawa “

====== TANZANIA ======

Katika MAISHA kila mtu ana kitu moyo wake unapenda, mara nyingine ama kwa kujua ama kwa kutokujua wengine wamekuwa hawaitendei haki MIOYO yao kwa kusikia / kusukumwa na sauti za nje (walimwengu).

Ukiona :

– Mtu ana maisha aina fulani mpotezee / jifunze / mshauri

– Mtu anakula mboga mboga badala ya Kuku, Bata na vile vitu vya Kontena na kwa mama Kamche… mpotezee / jifunze / mshauri

– Mtu anatumia Siemens C 25 (Zilipendwa) kama ya kwangu… mpotezee / jifunze / mshauri

Wakati mwingine tunachosha MISULI YA UBONGO kufikiri HASI kuhusu WATU na VITU badala ya kutumia muda mwingi wa thamani kwa kufikiri juu ya MAJIBU YA MATATIZO / CHANGAMOTO za Dunia ambazo kwazo waweza kuzigeuza FURSA zitakazokupelekea kukamata MSHIKO (PESA / UTATUZI wa Changamoto).

Siku moja Mwaka 1996 kama sikosei nilimtembelea Baba yangu Mdogo Mr. Canaan Msigwa nyumbani kwake alipenda kupiga Kaseti ya wimbo KIPENDA ROHO hula nyama mbichi… ule msemo ulinikaa siku zote na kunifanya wakati wote niusikilize kwanza MOYO wangu (Mtu wa Ndani yangu) kabla ya watu wa nje.

Songa mbele

Jiamini

Jithamini

Jitambue

========== ASANTE =========

@ BAGATECH

Godwin D. Msigwa

Qingdao

China

23 April 2019

Share.

About Author

Leave A Reply