Sunday, August 25

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA UZINDUZI WA VITUO SITA VYA POLISI VINAVYOHAMISHIKA

0


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, kukagua mazingira ya ndani ya moja kati ya Vituo vya Polisi Vinavyohamishika baada ya kuzinduliwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri huyo lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ahmada Khamis(kulia), baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, lengo ikiwa ni usogezaji karibu wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Katikati ni Mkuu wa Shirika linaloshughulika na Usafirishaji wa Wakimbizi nchini (IOM), Dk. Qasim Sufi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali ya Waandishi wa Habari baada ya Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni usogezaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi na wageni waalikwa baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika, lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi kwa wananchi. Waliosimama ni Kikundi cha Polisi Jamii cha Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.