Tuesday, August 20

MAONI YA MSOMAJI: KUHUSU KIFO CHA AQWILINA AKWILINE

0


Ninalazimika kuweka mawazo yangu kuhusu msiba wa mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji (NIT), Aqwilina Akwiline aliyeuwawa kwa risasi akiwa kwenye chombo cha usafiri (daladala).

Napenda kuweka hapa facts zifuatazo:

1. Kila siku Kinondoni zinapita daladala nyingi.

2. Daladala nyingi zilipita wakati wa kampeni Kinondoni.

3. Kwenye daladala hizo, huwa kuna abiria wengi; wengine huwa wamesimama kwa kukosa nafasi za kukaa.

4. Siku aliyofariki mwanafunzi huyu, alifariki kwa risasi moja ambayo kwa bahati mbaya ilimpiga kichwani. Risasi hiyo haikumpiga mtu mwengine yeyote isipokuwa mwanafunzi huyo. Ninalazimika kuamini kwamba aliyefyatua risasi hiyo hakukusudia kumpiga mwanafunzi huyo.

5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa tamko linaloagiza waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

6. Uchunguzi unaendelea utakaobaini ni nani aliyefyatua risasi hiyo ya moto iliyopelekea kupotea kwa roho ya mwanafunzi huyu. Umma utaarifiwa matokeo ya uchunguzi huo.

7. Kiti hicho ambacho kinaweza kuonekana ni tukio is bahati mbaya kimegeuzwa gumzo kubwa la siasa la is kumtuhumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali anayoiongoza ya awamu ya 5. Haistaajabishi kwa wapinzani kutafuta sababu za kuipaka matope serikali na chama tawala, ila kwa suala la kibinadamu kama hili; tulipaswa kuwafariji wafiwa pamoja na kuhimiza kukamilishwa kwa uchunguzi. Mheshimiwa Waziri wa Elimu ashaelezea kwa kirefu maoni ya Wizara yake na hatua stahiki zitakazochukuliwa. Wazungumzaji wa Jeshi la Polisi nao washaelezea. Nadhani sio busara kukuza munkari kwa jambo hili; marehemu hakua katika harakati za siasa.

MWISHO

Nakuombeni Watanzania wenzangu tuangalie masuala muhimu yaliyo mbele yetu. Hili la mwanafunzi tushiriki katika maziko na tusubiri uchunguzi ukamilike.

Ni Mimi Dr. Abdullah Makame.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.