Wednesday, August 21

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA YAZIFUTIA LESENI KAMPUNI NNE ZA USHAURI NA UDALALI WA BIMA

0


Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza agizo la kuzifutia leseni za makampuni manne ya Ushauri na Udalali wa bima (Insurance Brokers) kwa kukiuka malengo ya leseni zao. Picha na Cathbert Kajuna.

Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)imeamua kuzifutia leseni za kampuni nne za ushauri na udalali wa bima (Insurance Brokers).

Akizungumza leo Dar es Salaam, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware amesema kampuni hizo za udalali na ushauri wa Bima yaliyofungiwa yalikuwa yamesajiliwa na kupewa leseni ya kufanya biashara ya bima kwa mujibu wa sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009.

Ametaja kampuni ambazo zimefutiwa leseni ya udalali wa bima ni kampuni ya udalali wa Bima ya HANS, ENDEAVOUR, LEGEND OF EAST AFRICA, pamoja na SWIFT.

Kamishna Dk.Saqware ameongeza kapuni hizo zimefungiwa kwa kosa la kutowasilisha ada za bima kwa kampuni ya bima ambapo mawakili wa kampuni wamefunga ofisi bila kulipa ada stahiki na kufuta taratibu zilizowekwa za kufunga ofisi.

Aidha amesema mamlaka imetathimini mwenendo wa kampuni hizo na kuona ni vema ikachukua hatua za haraka zilizo ndani ya uwezo wake kwa mujibu wa sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 kifungu cha 74, ambayo ni kuyafutia leseni ya biashara kampuni hizo.

Dk.Baghayo amesema kinachotakuwa ni kuhakikisha wateja wa Bima kupata haki na heshima ya soko hilo inalindwa hata baada ya kampuni hizo kufutiwa leseni.

Amewataka wananchi kutambua uwepo wa mamlaka ya usimamizi wa shghuli za Bima hapa Nchini.”

Wananchi wasilalamike na kunung’unika pale wanapopata matatizo ya kibima na kwa kutokuja wapi pa kwenda.

“Mamlaka kupitia ofisi zetu za makao makuu na katika kanda za Nyanda za juu kusini (Mbeya jengo ka NHC-mtaa wa Lupa), kanda ya kati (Dodoma)katika jengo la LAPF-mataa wa Makole, kanda ya ziwa (Mwanza :jengo la PPF Bara bara ya Kenyatta) na kanada ya Kaskazini (Arusha :jengo la NSSF-Mataa wa Kaloleni).

“Pia kuna Kanda ya Pwani (Dar es Salaam) na ofisi ya Mamlaka ya Visiwani Zanzibar katika jengo la TIRA Mtaa wa Kilimani)tuko tayari kusikiliza kila mwananchi.Mamlaka iko imara katika kuhakikisha Sekta za bima nchini inakuwa sehemu za chachu ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla,”amesema.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa sheria mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Magreth Mngumi ametoa mwito kwa watanzania kuwa na imani na mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini na wateja waendelee kufurahia huduma zao ili kongezeka pato la taifa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.