Wednesday, August 21

LYANIVA KUTATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA TANDIKA

0


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Tandika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Tandika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva aongea na wafanyabiashara wa Tandika na kuwaahidi kutatua kero zinazowapata pindi wawapo katika biashara zao.

Aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maeneo yanayotoa huduma za jamii katika wilaya ya Temeke. Lyaniva aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa ataondoa kero zote zinazolikumba soko hilo .

Moja ya kero kubwa inayoikumba soko hilo ni miundo mbinu inayoizunguka soko hilo, ikiwemo kutuama kwa maji kipindi cha mvua. Lyaniva awaahidi kuwa atashughulikia kero hizo ili kuhakikisha mahali hapo panakua salama kwaajili ya kutoa huduma za kijamii.

Katika ziara hiyo aliambatana na katibu Tawala wilaya,watumishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,diwani wa Tandika,wenyeviti wa Mitaa,wakuu wa vyama vya siasa mbalimbali,wajumbe wa Mitaa,afisa Tarafa Chang’ombe na wadau wa utoaji huduma za jamii mbalimbali ikiwemo TARURA,TAKUKURU,DAWASCO na TRA.

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya alielekea ofisi ya kata ya Tandika ambapo alifanya kikao cha wadau wa maendeleo na wananchi. Ambapo alisisitiza kuhakikisha wanafunzi wote waliofauru darasa la saba 2017 kama wameripoti shuleni. Aliwaasa wazazi kutoa ushirikiano ili watoto wao wasibaki nyumbani kujiingiza katika makundi hatarishi.

Hata hivyo Lyaniva aliwataka wananchi kutoa kiwango stahiki cha kuzoa takataka ili kusaidia zoezi la ukusanyaji taka kuwa rahisi. Pia alisisitiza usafi wa kila jumamosi kwa wananchi wote ni lazima.
Pia aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya jamii inayotolewa na serikali kwa riba nafuu kupitia benki ya DCB. Wakinamama na vijana wamehamasishwa kwenda kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua katika hali ya kiuchumi na jamii.

Lyaniva alisisitiza kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo endapo mwananchi atakutana na mazingira yoyote ya rushwa atoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU Wilaya ili hatua kali za kisheria zichukuliwe. Alisema huduma za jamii ni bure kwa kila mtu hivyo wananchi wasiruhusu vitendo vya rushwa.

Aidha aliwataka wananchi kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ili kuiongezea mapato serikali,na kwa mapato hayo hayo yatasaidia kuboresha huduma za jamii.

Ziara hiyo ya mkuu wa wilaya yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo katika jamii itaendelea katika kata zote zilizopo wilaya ya Temeke katika vipindi tofauti tofauti.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.