Sunday, August 18

KAMPUNI ZA BIMA ZATAKIWA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA UWAZI

0


Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA, Bw. Elia Kajiba akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wa Bima uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.

Kampuni za bima nchini zimeshauriwa kuwahudua wananchi kwa uwazi na kutoa huduma za kiwango cha juu ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba wakati mkutano wa wadau bima ulioandaliwa African Insurance Digital Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa bima imeanzishwa kwa ajili ya kulinda biashara na mali hivyo wananchi wanatakiwa kuhudumiwa katika kulinda biashara na mali zao huku wakitoa elimu kwa uwazi.

Aliongeza kuwa mtu mwenye bima katika biashara au mali likitokea janga haiwezi kuwa sifuri kutokana na kukata bima kwa ajili ya biashara na mali hizo.

“Kampuni za Bima ili ziweze kufanya kazi ni lazima zisajiliwe katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi,” alisema.

Alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda sekta ya bima zina mchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi.

Nae Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.

Mtavangu alisema kuwa lengo lingine kuu la mkutano wa kuwakutanisha ni wadau ni pamoja na kujadili changamoto zinazowazunguka watoa huduma wa bima kuweza kujadili kwa nia ya kuboresha utoaji wa Bima kwa wananchi.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema mkutano huo wameuandaa katika kipindi mwafaka katika kwenda na dhamira ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo watoa huduma wa bima ndiyo fursa ya kufanya kazi na viwanda hivyo katika utoaji wa bima.

“Tutaendelea kufanya mikutano zaidi ili katika kuwaweka watoa huduma wa bima kuwa karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa maonesho ambapo wananchi wanaweza kupata huduma za bima,” alisema.

Mkutano huo wa pili wa masuala ya BIMA, ilisema kuenda pamoja na maoneshi ya Bima kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo.

Nchi zipatazo Tano zimewesha kushiriki katika mkutano huo ni Rwanda, Kenya, Afika Kusini, Nigeria na Tanzania ambao ndiyo wenyeji wa mkutano.

Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Bima nchini, Sam Kamanga aliyaomba makampuni ya bima kuendelea kutoa bima kwa uaminifu na uwazi mkubwa ili kuweza kujijengea heshima katika jamii.

“Nawaomba watoa huduma zote muwe wawazi, na huduma zenu ziwe za kiwango cha juu maana tumekuwa tukipata malalamiko mengi toka kwa wananchi juu ya uzembe mchache ambao umekuwa ukifanywa na kampuni ambazo si waaminifu, hivyo lazima tufuate sheria na kanuni tulizojiwekea,” alisema.

Alisema kuwa uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya Bima hivyo wasipokuwa waaminifu watashindwa kuhudumia viwanda na taifa likatapa matokeo chanya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.