Friday, April 19

KAMPENZI YA ‘FURAHA YANGU’ YATEKELEZWA VYEMA NA WATUMSHI WA WIZARA YA HABARI

0


 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Prisca Shewali akifanya kipimo cha VVU katika zoezi la upimaji wa afya lililokuwa likifanyika leo katika Ofisi za Wizara kwa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” kushoto ni Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Makole Jijini Dodoma Hadasa Haruni.

Na Anitha Jonas – WHUSM.

 Afisa Bunge Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Francis Songoro akifanya kipimo cha VVU katika zoezi la upimaji wa afya lililokuwa likifanyika leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma kwa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” kushoto ni Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Makole Bibi.Hadasa Haruni.

 Katibu Muhtasi Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Niuka Chande akipima Shinikizo la Damu wakati wa zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi wa wizara kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” lililokuwa likiendelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma na wataalamu kutoka Hospitali ya Makole (kushoto ) Daktari Janeth Mtenga.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika foleni ya kupima afya zao wakati wa zoezi la upimaji wa afya kazini kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” lililokuwa likiendelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Share.

About Author

Leave A Reply