Wednesday, August 21

IFAD KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO

0


Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa ukuaji wa Sekta ya Kilimo kwa takribani asilimia 6, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika, wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga. 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akizungumza kuhusu Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kusaidia katika kutoa mikopo ili kuwasaidia wakulima kuwa na kilimo endelevu wakati wa Mkutano na Rais wa IFAD Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga na kulia ni Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Mgonya Benedicto.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Ujumbe wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo (kulia), ukiwa katika mkutano ulioangazia Maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini na namna ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, baada ya Mkutano ulioangazia maendeleo ya sekta ya kilimo nchini na namna ya kutatua changamoto zake, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na mgeni wake Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, akipokewa na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga (kulia), alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma kwa ajili ya mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa sita kushoto) na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo (wa sita kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania na IFAD, baada ya kumalizika kwa mkutano ulioangazia Maendeleo ya Sekta ya Kilimo kikiwemo kilimo cha umwagiliaji, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

Share.

About Author

Leave A Reply