Saturday, August 17

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AAGIZA UCHUNGUZI KIFO CHA KIONGOZI WA CHADEMA

0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Hananasifu, Daniel John yaliyotokea Kinondoni, Dar es Salaam.

Alitoa maagizo hayo jana katika Kata ya Kasindaga Wilaya ya Muleba mkoani Kagera katika uzinduzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya taifa mkoani humo. 

Alisema ni vyema jeshi la polisi lichunguze kwa kina tukio hilo na kujua undani wake na kuwaeleza wananchi chanzo cha mauaji hayo na hatua zinazochukuliwa.

“Mataifa mengine mtu akiuawa shughuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu kupoteapotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu na kuona ni jambo la kawaida tu, lazima mfanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,” alisema Dk Mwigulu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.