Thursday, August 22

RAIS ANAYEPENDA KUSAFIRI NA KWENDA ZAIDI MATAIFA YA KIGENI AFRIKA

0Rais wa Cameroon Paul Biya amekuwa madarakani kwa takriban miaka 35. Lakini utawala wake wa miaka mingi umekuwa gumzo nyumbani , muda anaotumia akiwa katika mataifa ya kigeni umezua hisia za kimataifa.

Akikosolewa na wengine kutokana na uongozi wake wa kuwa nje ya taifa , rais Paul Biya wa Cameroon hivi karibuni aliitisha mkutano wa baraza lake la mawaziri kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka miwili.

Uchaguzi wa urais hufanyika mwezi Oktoba na raia wa Cameroon husubiri kusikiza iwapo rais huyo mwenye umri wa miaka 85 atawania muhula mwengine.

Lakini hakuna tangazo kama hilo lililofanywa katika mkutano huo. Bwana Biya amekuwa uongozini tangu 1982, akiwa ni miongoni mwa viongozi wa bara Afrika walioongoza kwa muda mrefu .

Chini ya uongozi wake Cameroon imenusurika mgogoro wa kiuchumi kabla ya kubadilika kutoka kuwa taifa la chama kimoja hadi kuwa na vyama vingi.

Lakini pia taifa hilo limekumbwa na ufisadi wa kiwango cha juu mbali na kuzorota kwa uhuru wa kidemokrasia uliopatikana na kufutiliwa mbali kwa muda wa kipindi cha rais mwaka 2008 ambao ulimruhusu mzee huyo kuwania tena urais mwaka 2011. Rais Biya amekuwa nchini China wiki hii

Bara la Afrika la leo linabadilika .Kipindi cha viongozi walioongoza bara hilo kwa miongo kadhaa kinaendelea kuyoyoma .

Runinga zinazotumia setlaiti na mtandao umekuwa ukiwaelezea raia mabadiliko ya kidemokrasi katika mataifa mengine ya jangwa la Sahara.

Asilimia 60 ya raia wa Cameroon wako chini ya umri wa miaka 25 na hawakuwa wamezaliwa wakati Paul Biya alipochukua madaraka.

Kuna shinikizo kuu ya ajira na maisha mazuri. Chama cha upinzani cha Social Democratic Front sasa kimetambua ukweli huo.

Mapema mwaka huu kiongozi wa chama hicho John Fru Ndi, 76 alijiondoa na kumwachia mgombea mpya mfanyibiashara mwenye umri wa miaka 49 na rubani wa zamani Joshua Osih.
Hoteli ya Uswizi

Hii ndio changomoto inayomkumba bwana Biya huku akiamua iwapo atasimama kwa awamu nyengine ambayo itamfanya kuongoza muhula mwengine wa nne madarakani katika taifa ambalo linataka mabadiliko.

Kutokuwepo kwake katika taifa hilo kumewafanya wakosoaji wake kutoa hisia kali dhidi yake.

Safari zake za kigeni zimesababisha makabiliano ya mtandaoni kati ya gazeti la Tribune na mradi wa uhalifu unaopangwa na Ufisadi OCCRP ambao ulihesabu muda unaotumiwa na rais huyo ugenini kwa kutumia ripoti za magazeti ya kila siku.

Mradi huo wa kukabiliana na ufisadi na ripoti za uhalifu unakadiria kwamba rais alitumia takriban siku 60 nje ya taifa hilo mwaka uliopita katika ziara za kibinafsi.

Pia imedaiwa kwamba alitumia thuluthi moja ya mwaka 2006 na 2009 ughaibuni.

Hoteli ya Intercontinental mjini Geneva ndio imedaiwa kuwa anayoipenda. Gazeti hilo linalomilikiwa na serikali lilitaja uchunguzi uliofanywa kuwa propanganda za uchaguzi. Wachezaji wa timu ya soka ya Cameroon wakimsalimia rais Biya na mkewe Chantal ili kuigiza salamu za mzaha

Nyumbani, rais amekuwa haonekani hadharani na mara nyengine huelekea nyumbani kwake mashambani.

Huamini uongozi wa kila siku serikalini wa waziri wake mkuu Philemon Yang ambaye hufanya mikutano ya kila mwezi ya baraza la mawaziri. Waziri huyo mkuu hupewa uwezo mkubwa wa kusimamia kazi za kundi lake la mawaziri huku rais huyo akikutana na viongozi wakuu kibinafsi katika makao ya rais katika mji mkuu wa Younde.

Mtindo wa rais Biya kuliongoza taifa hilo akiwa ughaibuni umewafanya wakosoaji wake kuzungumza kuhusu ”rais anayeongoza akiwa ugenini”.

Rais Biya kama mtangulizi wake Ahmadou Ahidjo anatoka katika jimbo la raia wanaozungumza Kifaransa huku waziri mkuu akitoka jimbo la raia wanaozungumza Kiingereza.

Rais lazima aonekane akiongoza serikali ili kuendelea na kazi yake kulingana na mchanganuzi wa Cameroon ambaye hapendelei upande wowote.

Kwa hivyo wakati rais Biya anapokutana na mawaziri wake kwa mkutano wa baraza la mawaziri usio wa kawaida ni kutokana na sababau maalum.

Mkutano wa hivi karibuni kufanyika ni ule wa kundi jipya la mawaziri baada ya mabadiliko mapema mwezi huu.

Ni sawa na mkutano wa mwisho wa baraza la mawaziri ,2015 ambao ulifanyika mara tu baada ya mabadilliko.

Wakati huo kulikuwa na uvumi kwamba rais Biya atatangaza iwapo atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu, ili kuongoza muhula mwengine lakini hakutoa ishara kuhusu swala hilo.

Licha ya kwamba barazo la mawaziri lilikuwa muhimu.

Maswala ya Lugha.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja , jimbo la raia wanaozungumza lugha ya Kiingereza nchini Ufaransa kaskazini magharibi na kusini magharibi limezongwa na mgogoro.

Hii ilianza kama maandamano ya mawakili na walimu wakitaka lugha ya Kiingereza kupewa fursa ya kutumika.

Lakini wasiwasi ulizuka, na kusababisha makabiliano kati ya vikosi vya usalama ,kukatwa kwa mtandao kwa takriban siku 93 katika jimbo la raia wanaozungumza Kiingereza nchini humo huku watu wanaojitenga wakipigania jimbo lao la ‘Ambazonia’ huku kukiwa na idadi kubwa ya vifo kutoka pande zote mbili.

Serikali ilichukua hatua kuangazia swala hilo lakini hali bado inaonekana kuwa hatari.

Mataifa ya Uingereza na Ufaransa yametaka kufanyika kwa mazungumzo. Rais Biya alijibu kwa kuunda baraza jipya la mawaziri tarehe 2 Machi .

Udhabiti wa usalama na amani uliimarishwa kupitia uundaji wa wizara ya ugatuzi ikitoa ahadi ya kuleta maendeleo mashinani mbali na huduma kwa raia. Jimbo la Ksakzini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Cameroon yanazungumza kiingereza

Alitumia baraza hilo lisilo la kawaida ili kuonyesha anavyowaunga mkono mawaziri wake mbali na kutumna mpango kuhusu uthabiti wa usalama katika eneo lenye utata la raia wanaozungumza Kiingereza , lakini pia kugatua mamlaka ili kuwapatia raia uwezo wa kusimamia maswala yao.

Hivyobasi rais huyo anayeongoza kutoka ughaibuni amekuwa akionyesha uthabiti wa uongozi wake huku akijiandaa kuachilia madaraka.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.