Monday, August 19

MAKTABA YA MKOA WA MOROGORO YAPIGWA JEKI NA KOICA

0
Mkurugenzi mkazi wa shirika la misaada la Korea nchini (Koica), Joonsun Park akimsikiliza Mkutubi wa kujitolea wa nchi hiyo, Bi Ha Young (katikati) akimweleza jambo wakati wa hafla ya shirika hilo la kadhibidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh5 milioni vikiwemo vitabu 276 katika maktaba ya mkoa wa Morogoro, kushoto ni Mkutubi wa mkoa huo, Edward Fungo. Picha na Juma Mtanda.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
Morogoro. Maktaba ya mkoa wa Morogoro imepokea msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitabu 276 vya kiada vyenye thamani ya sh3.6 milioni baada ya shirika lisilo la kiserila la nchini Korea (Koica) kusaidia zaidi ya sh5 milioni katika kipindi cha miaka mitatu kutoka mwaka 2016/2018 katika maktaa hiyo mkoani hapa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mjini hapa, Mkutubi wa kujitolea, Bi Ha Young alisema kuwa Koica tayari imesaidia zaidi ya sh 5 milioni katika mambo mbalimbali katika maktaba ya mkoa wa Morogoro kwa miaka mitatu.

Bi Ha alitaja msaada huo kuwa ni pamoja na ununuzi wa jumla ya vitabu vya kiada 276 vyenye thamani ya sh3,695,500 milioni, kujenga vimbwete vinne (Meza) vyenye thamani ya sh 1,479,000 milioni, ukarabati wa dali la maktaba hiyo sh256,100, meza sh500,000, kamera za ulinzi (CCTC) sh1,025,000 na vitu vingine vyote vikigharibu gharama dola 2645 za Marekani.

“Mimi ni mkutubi na nimekuja Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi ya kujitolea maktaba ya mkoa wa Morogoro lakini nilipofika hapa Juni 2016 niliona kuna mapungufu mengi ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya vitabu vya kiada kwa shule za sekondari na msingi lakini niliomba fedha Koica na kusaidia hii maktaba.”alisema Ha.

Mkutubi wa mkoa wa Morogoro, Edward Fungo alisema kuwa wamepata faraja kubwa kutoka kwa, Bi Ha Young pamoja na Koica kwa kuweza kusaidia mambo mbalimbali yaliyoweza kupunguza sehemu za changamoto katika maktaba ya mkoa.

Fungo alisema kuwa maktaba hiyo ilikuwa na vitabu vichache lakini uwepo wa vitabu 276 umesaidia kuwavutia wasomaji wengi wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari.

“Yapo mambo tunashukuru yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu, awali kulikuwa na wizi wa vitabu na mabegi lakini baada ya kuwekwa kamera za ulinzi tumekomesha tabia ya wizi kwani baadhi ya watu walikuwa na tabia ya kuiba mabegi na vitabu.”alisema Fungo.

Fungo aliongeza kwa kusema kuwa Koica imesaidia mambo muhimu yapo hawajamaliza yote pamoja na Bi Ha Young kufundisha watumishi wa maktaba program mbalimbali za kompyuta na idara hiyo imewavutia na watumishi wengine hasa manesi kuvutiwa kujifunza kompyuta.

“Ujio wa Bi Ha Young umesaidia mambo mengi kwa kusaidia kutafsiri vitabu vya lugha ya Kingereza kwenda Kiswahili na amefanya kazi katika maktaba ya watoto, idara ya rejea, idara ya kujiandikisha na kuazima, idara ya kurudisha vitabu, ufundi pamoja na Tehama.”alisema Fungo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi shirika la Korea la Koica, Joonsung Park amesema Korea itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali huku akituma ujumbe kwa raia wa nchini wanaokuja afrika kuja Tanzania na kujikita upande wa elimu. 

Park alisema kuwa Bi Ha Young awe balozi nzuri wa Koica nchini Korea kwa kuwaeleza raia wanaokuja kujitolea afrika waende Tanzania na kuingia upande wa elimu hasa katika maktaba.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.