Thursday, August 22

ALIYEKUWA MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ASAKWA NA TAKUKURU

0WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mtwara, Stephen Mafipa kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, Fortunatus Kagoro kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Mbali na Kagoro pia Kaimu Mweka Hazina, Heri Hamad, Ofisa Mipango, Theresia Nsumba nao ameagiza wakamatwe na baada ya uchunguzi watakaobainika kwamba hawajahusika na ubadhirifu huo watarudishwa kazini.

“Lazima fedha za Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa.”

Watendaji hao wanadaiwa kutumia Sh bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa kuchora mchoro na kujenga msingi katika maeneo mawili tofauti.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Masasi na Halmashauri ya wilaya ya Masasi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Alisema mwaka 2014 Serikali ilipeleka Sh milioni 575 wilaya Masasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri hiyo na fedha hizo ziliishia kutumika katika hatua za maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kutengeneza michoro ya jengo.

Waziri Mkuu amesema 2016/2017 Serikali ilipeleka tena Sh bilioni 1.25 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo Halmashauri hiyo ilikwenda kutafuta eneo lingine na kufanya tena shughuli zilizokuwa zimefanyika na kuanza ujenzi ambao umeishia katika msingi na fedha zimeisha.

Pia amewataka watendaji hao kutotumia fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuziba pengo la fedha za mradi huo ambazo baadhi yake hazijulikani zilipo na amewaagiza Madiwani kutoruhusu jambo hilo.

“Madiwani msikubali kutumia fedha za makusanyo ya ndani kupeleka kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo ambayo tayari Serikali ilishatoa fedha ya ujenzi wake,” alisema.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.