Monday, June 17

WABUNGE WATAKIWA KUACHA TABIA YAZUNGUMZA KWA NGUVU BUNGENI

0


Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amewasihi wabunge kuacha tabia ya kuzungumza kwa nguvu Bungeni wakati ambapo mbunge anachangia hoja kwakuwa hali hiyo husababisha baadhi ya wabunge kupoteza umakini wa kusikiliza michango ya wenzao.

Spika Ndugai amesema hayo leo Juni 5, 2018, Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, na kuwataka wabunge wa hasa wanaokaa upande wa chama tawala CCM kupunguza sauti za mazungumzo na kuongeza kuwa hawakatazwi kuzungumza lakini wanapaswa kutumia sauti za chini ili kuweza kusikilizana “Waheshimiwa wabunge hasa upande huu wa CCM mnaongea sana, hamumsikilizi hata mwezenu, nawaomba sana sauti zipungue, hukatazwi kuzungumza na mtu, lakini hata wewe mwenyewe ukisikiliza katika masikio utaona haina raha, tuwape nafasi wanaotaka kusikiliza wasikilize” amesema Ndugai. Spika Ndugai, alilazimika kukatisha kwa muda uchangiaji wa hoja za Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu, baada ya kuzidi kwa sauti ya mazungumzo na hivyo kuleta hali ya kutosikika kwa kwa hoja za mchangiaji. Bunge linaendelea na uchangiaji wa hoja mjadala wa mapitio ya mapato na matumizi ya Wizara ya fedha na mipango katika mwaka wa fedha 2018/2018 ambapo jumla ya shilingi trilioni 12.5 inatarajiwa kuizinishwa na Bunge hilo,Read More

Share.

About Author

Comments are closed.