Monday, June 17

WABUNGE WA UPINZANI WAFANANISHWA NA MBWA

0


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Job Ndugai amelazimika kumpokonya Najma Giga uongozi wa kikao cha Bunge baada ya mzozo uliosababbishwa na Mbunge wa CCM aliyewafananisha wabunge wa upinzani na Mbwa.

Ndugai amelazimika kuingia Bungeni kuongoza kikao kufuatia wabunge wa kambi ya rasmi ya upinzani kuanza kupiga kelele kupinga kauli iliyotolewa na mbunge wa Jang’ombe, Ali Hassan Omar wakati wa kikao cha 44 cha mkutano wa kumi na moja wa Bunge wa kujadili hotuba ya bajeti ya mwaka 2018/19 ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Mbunge huyo wa Jang’ombe amesema kuwa ukiona majuha wanapongezana wakaona wamefanya la maana, kuna Mbwa kama watatolewa bungeni itakuwa vizuri sana.
“Nasikia milio ya Mbwa humu Bungeni, ukiwatoa itakuwa vizuri sana kwakuwa wanatupigia kelele humu ndani.”amesema Omar
Hata hivyo, Kauli hiyo ilipelekea wabunge wawili kutoka Chadema, Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo na Mchungaji Peter Msigwa wa jimbo la Iringa Mjini kusimama wakitaka utaratibu ufuatwe kwa mchangiaji kuomba radhi.
Giga alimruhusu Ali Hassan Omar kuendelea kuchangia kitendo ambacho kilipelekea wabunge wa upinzani kuendelea kupiga kelele na wakati kelele zikiendelea na utulivu bungeni ukitoweka, Spika Ndugai akaingia na kuchukua uongozi wa kikao hivyo Giga aliyeanza kuongoza kikao hicho tangu asubuhi kulazimika kumuachia uongozi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.