Monday, June 17

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya mazingira duniani yatakayofanyika june 5 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva ambapo amewataka maafisa mazingira wa wilaya hiyo kuhakikishia wanafuata sheria za mazingira.
Amewataka maafisa hao kuondoa marundo ya takataka yaliyorundikwa sehemu mbalimbali za wilaya hiyo hasa zilizopo pembezoni mwa barabara.
“Nataka sheria ya mazingira itumike kutunza mazingira yetu, sitaki kuona takataka zimerundikwa pembezoni mwa barabara zilizopo kwenye Manispaa yangu, wahakikishe kuwa wao wanakuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi kuondoa takataka,”amesema Lyaniva
Hata hivyo, Lyaniva amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mazingira kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam na mgeni rasmi anatarajiwa rais Dkt. Magufuli.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.