Monday, June 24

MAANA YA NENO MAPENZI

0


Tumekuwa tukisia neno mapenzi likitumika kwa kwa watu namapenzi hayo yakihusisha baibna ya mtu na mtu, mtu na kitu na hata kwa mwenyezi mungu. Lakini tukiulizana maana ya halisi ya neno mapenzi hujikuta tukijikanyaga tukiwa hatuna majibu rasmi juu ya maana ya neno hilo.
Leo kupitia 360habari tunakujuza mana ya neon mapenz:
Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.
Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu ("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia.

Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usioelekea kabisa ngono[1] na hata umoja wa kina au ibada ya upendo wa kidini.
Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika Sanaa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.