Sunday, August 18

360 news

0


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema kuwa halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha mfanyabiashara ya machungwa, Allen Mapunda (20) anayedaiwa kufariki muda mfupi baada ya kuachiwa na polisi.

Hayo yamesemwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa jeshi hilo halihusiki na kifo hicho na kwamba amefungua jalada la uchunguzi kupitia ofisi ya upelelezi wa makosa ya jinai kwa ajili ya uchunguzi.
Amesema kuwa Machi 24, mwaka huu saa sita usiku, askari polisi waliokuwa katika operesheni ya kukamata wahalifu katika mtaa wa Airport kata ya Iyela jijini humo waliwakamata vijana 12 akiwemo Allen.
Aidha Mpinga ameongeza kuwa Machi 25, mwaka huu saa nne asubuhi alitoka mahabusu baada ya kudhaminiwa na ndugu zake na ilipofika saa 12 jioni zilipatikana taarifa kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia.
“Ivi kwa akili ya kawaida kijana katoka polisi anachiwa anakufa. Ukiwa na mgeni akitoka kwako akifa wa kuchunguzwa ni nani,”amesema Kamanda MpingaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.