Friday, August 23

360 news

0


Kufuatia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi, Abdul Nondo amesimamishwa masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), hadi pale kesi yake itakapoisha.

Nondo amesimamishwa masomo yake kuanzia March 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na kupigwa saini na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.
Hata hivyo tangu Nondo ashikiliwe na polisi kwa mara ya kwanza jana aliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5, na kesi yake kuhairishwa na imepangwa kusikilizwa tena mahakamani Aprili 10, 2018.
Nondo anashtakiwa kwa makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni kuwa yupo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa WhatsApp.
Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.