Sunday, August 25

360 news

0


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema hawezi kumzungumzia au kumshauri Mange Kimambi kwani hana uhakika kama ni binadamu wa kawaida.

Akizungumza katika kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Dkt. Tulia alisema kuwa hawezi kumshauri kitu mwanamke huyo maarufu kwenye mitandao ya kijamii kwani kwa kile anachosikia kuhusu anachokifanya mitandaoni ana mashaka ‘ni aina gani ya kiumbe wa binadamu’.
“Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua kitu cha kuzungumza naye,” alisema.
“Lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye,” aliongeza.
Aidha, Dkt. Tulia alisema kuwa hawezi kusema kama anachokifanya anakosea au yuko sahihi kwani inategemea yeye ni jamii gani ya binadamu (specie).
“Huenda hakosei, labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti. Hivyo, kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea,” Dkt. Tulia anakaririwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.