Thursday, August 22

WAKULIMA WAOMBA KIWANDA CHA KUCHAKATA VITUNGUU

0


Rais wa mfuko wa kimataifa na maendeleo ya kilimo (IFAD) Mhe. Gilbert Houngbo ametembelea ghala la wakulima wa vitunguu Mang’ola. Amejionea namna ghala la vitunguu linavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na wanachama wa Lake Eyasi Commercial Farmers Networks (LEKOFANET) ambao alitaka kufahamu kuhusu shughuli zao za kilimo. 

 Awali Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo ameshukuru IFAD kwa kujenga ghala la kuhifadhia vitunguu. Mhe. Theresia amesema ghala limejengwa kwa gharama ya shilingi billion 1.5, mradi wa barabara wa km 27 uliojengwa na Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance Support (MIVAF) billion 1.54 IFAD walijenga Barabara ya km 27. Mhe. Mahongo amesema Halmashauri ilichangia 5% kila mradi, halmashauri ilichangia million 74.4 kwenye mradi wa barabara na Mivarf ilichangia billion 1.4, Mradi wa ghala Halmashauri ilichangia million 76.5 na Mivarf ilichangia billion 1.4.

Mhe. Theresia amesema ghala limesaidia sana wakulima kuhifadhi vitungu ili vipande bei, amesema wakulima wa vitunguu Tarafa ya Eyasi wako takribani 1400. Amesema Mwaka 2017 wakati wanaanza kutumia ghala gunia la vitunguu kwa bei ya awali liliuzwa kwa sh.45000 lakini wakulima walipo hifadhi vitunguu kwenye ghala baadae waliuza gunia kwa sh 100000.wakulima hawa waliweza kupata mafunzo ya namna ya kujiendesha wenyewe na wameweza kuunda ushirika ambao uko katika hatua za mwisho ili waweze kusajiliwa. Mhe. Theresia amesema Karatu ni wanufaika wakubwa wa serikali ya awamu ya tano, serikali imetoa zaidi ya shilingi billion 5 kwa elimu bure tangu mwaka 2015 mpaka sasa. Lakini serikali imeweka lami kiasi cha km 0.6 kwa sasa Karatu mjini, Mhe.Theresia amesema serikali itaweka   lami Karatu  mjini km 10 na tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika.

Mhe. Ally Lorry mkazi wa Tarafa ya Eyasi amesema ghala limesaidia kuwaondolea matatizo waliokuwa wakiyapata hapo awali. Amesema kulikuwa kuna shida ya ubovu wa barabara zinazotoka mashambani, Mhe. Ally amemuomba Rais wa IFAD kuwatafutia wakulima masoko nje ya nchi,lakini pamoja na kuwatengenezea kiwanda cha kuchakata vitunguu ili zao la vitungu lipate bei nzuri zaidi.

Ndugu Gabriel Boay Mkazi wa Tarafa ya Eyasi amesema wao wanahitaji kupiga hatua katika kilimo cha vitunguu zaidi. Amesema ghala limewasaidia katika shughuli za kilimo cha vitunguu kwa kuongeza dhamani ya vitunguu. Barabara imesaidia kwa wafanyabisahara kutoka nje ya nchi kuja kununua kitunguu Mang’ola. Kutokana na uwekezaji huo wa miundo mbinu wakulima wametoka katika uchumi wa chini na kuelekea hatua ya uchumi wa katikakati.


Share.

About Author

Leave A Reply