Saturday, August 24

MANG’OLA TUACHE KUCHOMA MOTO VYANZO VYA MAJI .

0


Mkuu wa wilaya ya karatu Mhe. Theresia Mahongo amewakataza wananchi wa Tarafa ya Eyasi kuchoma moto katika chanzo cha maji Qangdend. amesema chanzo hicho kikiharibika wananchi wa mang’ola hawataendelea tena na shughuli za kilimo. Tangu juzi kuna moto unawaka katika chanzo hicho cha maji.

Mhe. Theresia amesema hayo katika sherehe za waguzi zilizofanyika katika kituo cha afya Mbuga Nyekundu. Wanaofanya hivyo ni sawa na kuwachoma sindano ya sumu, amesema yale matete na miti yanazuia jua kufyonza maji moja kwa moja. Ameomba watu wanaowafahamu watu wanaochoma moto watoe taarifa ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao. Kanda hii ya umwagiliaji kuna vijiji saba tunategemea chanzo kile cha maji ambacho kitakauka, serikali inapigania kuongeza maji kwa kuchimba visima ili maji yajitosheleze kwa kilimo cha umwagiliajia Mang’ola.

Mhe. Theresia amemuelekeza Katibu Tarafa kukaa na wenyeviti wa kijiji kutafuta ufumbuzi kwanini chanzo kile hakitunzwi. Mhe.Theresia amewataka pia JUWAMABOYE kuchagua uongozi mpya baada ya uongozi wa sasa kumaliza kipindi chake. Amesema kwa sasa kuchagua uongozi kwa ngazi ya kijiji umekamilika hivyo amewataka kumalizia kuchagua uongozi huo ili ukamilike ndani ya mwezi wa sita. Mhe. Theresia amesema amesikitishwa sana baada ya kusikia kwamba zinahitajika million kumi, Mhe. Theresia amesema sisi ni watumishi wa umma amehoji kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya matumizi gani ? Mh. Theresia amesema kazi hiyo ni lazima ifanyike.

Mhe. Theresia amesema ni marufuku kwa wafanyabishara kufunga rumbesa, amesema kufanya hivyo ni kuwanyonya wakulima. amewataka wakulima kukataa kufunga rumbesa, amesema wakulima wanalima kwa gharama kubwa halafu wanapata faida kidogo. Wakulima wanachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Karatu. Mhe. Theresia amemuagiza Katibu tarafa kuwakamata watu wanaojaza rumbesa, na amesema kutakuwa na kizuizi cha kukagua katika geti la manyara na kuweka kizuizi pia barabara ya Mbulumbulu. Mhe Mahongo amesema kuliko kujaza rumbesa bora waende wakahifadhi mazao kwenye ghala, ili kusubiri bei imarike. Amesema serikali inapigana kutafuta masoko ya mazao, na wameshazungumza na Rais wa IFAD juu kupata soko zuri la vitunguu na wakati alipofanya ziara wilayani Karatu.


Share.

About Author

Leave A Reply