Monday, August 26

WAZIRI KAMWELWE ATOWA MAAGIZO KWA TANROADS

0


Na George
Mwigulu,Katavi .

  Waziri  wa  Ujenzi  Uchukuzi na 
Mawasiliano Mhadisi Izack  Kamwelwe amewaagiza Wakala wa Barabara 
Tanzania ( TANROADS)   wawe  na  mkakati  mahsusi
  wa usimamizi  bora  wa  mizani za kupimia magari 
ili kupunguza  kero na malalamko  kwa wasafirishaji  na
watumiaji wengine.

 Mhadisi Kamwelwe ametowa maagizo  hayo hapo jana
wakati alipokuwa akifungua mkutano wa kumi na 12 wa  baraza la Wafanyakazi
wa ( TANROADS) uliofanyika katika ukumbi wa  Polisi  
katika  Manispaa ya    Mpanda  Mkoani  Katavi .

  Mbali ya  agizo hilo  ameelekeza 
mambo yafuatayo yafanyike  ili TANROADS   iweze kuendelea 
na kasi  ya  Serikali ya awamu ya tano  katika kutekeleza 
ilani ya  uchuguzi .

 Aliwataka  wahakikishe  miradi yote 
inayoendelea  na ujenzi  inakamilika  kwa wakati  na kwa
ubora   unao tarajiwa .

 Baadhi ya miradi wanayoisimamia  ijengwe 
kwa mfumo  wa  Desgin and  Build ili  iweze 
kwenda  kwa haraka na kumalizika kabla ya  wakati

 PIa  wasimamie  kwa  karibu 
mikataba  ya kazi  baina  ya   Makandarasi  na
wafanyakazi  wazawa  kwenye miradi yote ya ujenzi inayofanyika 
hapa  nchini .

 Waziri   Kamwelwe  aliwasisitiza 
waweke  utaratibu  kwa kila mkandarasi   anaekuwa ameoewa mradi
wa ujenzi  achangie huduma  za jamii ( Corporate Social
Responsibillty.) kwenye maeneo ya  miradi ya ujenzi 
inapotekelezwa  na kuandaa  mafunzo  ya mara kwa mara  kwa
kada zote  ili kuwasaidia watumishi  kuendana na mabadiliko  ya
technolojia  na matumizi  ya Tehama kwenye kazi .

 Nae   Katibu   Mkuu wa  
Ujenzi  Elius  Mwakalinga  alisema hivi karibuni Bunge 
ililipitisha  Bajeti  ya Wizara  pamoja na ukweli 
kwamba  fedha iliyopitishwa  kwenye  miradi ya Maendeleo 
siyo kubwa  kama  ambavyo  walivyopendekeza .

 Hivyo aliwataka  isiwavunje nguvu ya kufanya
kazi  ya kusimamia  na kukamilisha miradi  mbambali ya 
maendeleo  anafahamu kuwa  ipo Mikoa   
ambayoimetengewa  fedha kidogo  za matengenezo ya barabara .

 Lakini rai yake kwa Tanroads  ni wajipange 
sasa  kuweza  kutumia  kiasi  kilichotengwa cha fedha 
kuweza  kufanikisha   malengo  yao katika 
matengenezo  na  miradi  mbambali ya maendeleo 
hususani  miradi ya  barabara .

 Mtendaji  Mkuu wa 
Tanroads  Mhadisi Patrick  Mfugale  alisema kuwa 
Tanroads  walifanya vizuri  kwenye mradi wa ujenzi  wa
jengo  la tatu  la abiria  kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa  wa  Mwalimu  Julius  Nyerere wa  Dar es
salaam(JNIA TIII)   nandio maana wameaminiwa  kusimamia 
ujenzi  wa mradi wa kituo cha kufua umeme( Strieglirs  Gogle)
huko   Rufiji   Mkoani   Pwani .

 Na wao  kama  Tan roads wako tayari 
kusimia  mradi huo na miradi mingine watakayokuwa wamepewa na 
Serikali na watahakisha wanamaliza kwa wakati na  ubora unaotakiwa na
mradi kulingana   na gharama halisi ya pesa .

Share.

About Author

Leave A Reply