Tuesday, August 20

Wababe wa Simba sc wabaki ligi kuu

0


CEO wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amekiri Kuwepo kwa Makosa ya takwimu na kuirejesha timu ya Kagera suger katika ligi kuu ambapo sasa itacheza hatua ya play off huku klabu ya Stand United ya Shinyanga ikiwa imeshuka moja moja.

Wambura amesema kwa Makosa hayo ofisi yake inawajibika kwa kuomba radhi kwa mkanganyiko huo na kumpa adhabu aliyepotosha takwimu hiyo. Sasa rasmi African Lyon na Stand United zimeshuka moja kwa moja huku Kagera Sugar na Mwadui FC zitacheza Play Off na timu za Geita Gold na Pamba SC.


Share.

About Author

Leave A Reply