Monday, August 19

“VIONGOZI WA DINI LINDENI AMANI YETU”, WAZIRI MKUU MAJALIWA.

0


Dodoma. Leo Machi 31, 2018, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini kuhakikisha wanailinda na kuipigania amani ya nchi, na kuepuka kutoa matamko ambayo yanaweza kuligawa taifa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwa chachu ya amani na kutumia nafasi waliyonayo katika jamii kwa kuwashawishi Watanzania kudumisha amani ambayo ni tunu toka kwa mwenyezi Mungu.

Katika mkutano huo, Waziri mkuu amesema kuwa dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya binadamu, nakutaja kuwa hiyo ndiyo sababu ya serikali kuheshimu na kutambua mchango wa dini zote katika kudumisha amani ya nchi.

Waziri Mkuu amehitimisha kwa kuwasisitiza viongozi wa BAKWATA kuhakikisha chombo hicho kinaendelea kuwa sehemu ya kuwaunganisha watanzania wa dini na rangi zote.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.