Saturday, August 24

SIDO KATAVI YATAJA UKWEPAJI WA KODI CHANZO NI UKOSEFU WA ELIMU

0


Na George Mwigulu,Katavi.

Imetajwa kuwa Ukosefu wa elimu ya kibiashara na ulipaji kodi kwa
baadhi ya wafanyabiashara hasa wamiliki wa viwanda vidogo Mkoani Katavi
wamesababisha hasara kwa serikali inayokana na ukwepaji kodi unaofanywa na
baadhi ya wafanyabiashara.

Ukwepaji kodi 
 umekithiri sana kwenye Mkoa huo ambapo  umeligusa Shirika la
kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)Mkoa wa Katavi kuazisha mpango mkakati wa
kuwakutanisha wadau wake pamoja na Mamlaka ya kukusanya Mapato(TRA)Mkoani humo
ili kutafuta mwarobani wa ukwepaji kodi na kufikia malengo ya juu ya
ukusanyaji.

Alizungumza hayo jana ofisini kwake Mtaa wa Mpanda Hoteli na Waadishi
wa Habari Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Katavi Salome Charles Mwasomola kuwa
kama shirika la kuhudumia viwanda wanalojukumu la kusimamia wadau wake kupata
elimu ya kutosha ili kuboresha biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Mwasomola alisema kuwa wameamua  kuwakutanisha wafanyabiashara na
TRA  kupitia mikutano na warsha za ndani zitakazo leta faida kubwa kwao
zitokanazo na kupatiwa elimu.

Alisema kuwa  faida zitokanazo na kupatiwa elimu  ni
kuwawezesha wafanyabiashara  kutambua wajibu wao wa kulipa kodi kwa
serikali,kuwafanya watambue faida zitokanazo na ulipaji kodi,namna ya
kujisajili kwenye mamulaka ya ukusanyaji kodi ili wapatiwe TIN namba za
biashara zao ikiwa pamoja na kuwafanya watambue athari zitokanazo na ukwepaji kodi
kwa serikali.

Aidha Wafanyabiashara kuona umuhimu wa kusajili biashara zao
BRELA,Kusajili majina ya biashara na walio na uhitaji wa kusajili makampuni
waweze kufanya hivyo.

Kaimu Meneja huyo alifafanua kuwa lengo lao kubwa kama SIDO ni
kuhakikisha wafanyabiashara na wajasiliamali wananufaika na biasharaza
zao,kutoa ushauri wa kibiashara,kutoa ushauri wa kiufundi kwa wanao hitaji
teknolojia yoyote ya uzalishaji au kama wanahitaji kubadili teknolojia
wanayotumia  sambamba na kuwaunganisha kupata masoko ya uhakika.

‘’Sisi kama Shirika lenye dhamana ya kusimamia viwanda vidogo,Tunalo
jukumu la kuona wafanyabiashara wanajikomboa kiuchumi sambamba na kuhakikisha
wafanyabiashara hao wanakuwa walipaji wazuri wa kodi’’Alisema.

Vilevile aliwataka wajasiliamali wadogo wajitokeze kuhitaji msaada
kutoka SIDO maana wako kwa ajili ya kuwahudumia pamoja na kuwawezesha kupata
mikopo midogo ya Tsh 500,000/-hadi Tsh 5,000,000/-ambayo riba yake ni nafuu na
kuwaunganisha na taasisi za kibeki kwa ajili ya kupata mikopo mikubwa.

SIDO katika mafanikio iliyoyapata tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017
Mkoani humo imefanikiwa kuwaunganisha wanafanyabiashara hasa wamiliki wa
viwanda kwa kutengeza kongano mbili ni ile ya wasindika mpunga ambao ni wenye
viwanda vya kukoboa mpunga na wajasiliamali wadogo wa dogo kwa kuwapatia
mafunzo mbali mbali ya kuongeza thamani biadhaa zao.

Hivyo pia  kutokana na agizo la serikali la kuhakikisha kila mkoa
kwa mwaka wanakuwa na viwanda mia moja,alisema kuwa wamejipanga kwa mwaka huu
kuwa na viwanda therathini.

Nao baadhi ya wamiliki wa viwanda Mkoa wa Katavi Sida Mareka,John
Mwandu,Alex Jipole,Mussa Khamis na Rashid Juma walisema kuwa ujio wa SIDO
Mkoani humu umekuwa chachu kubwa ya mafanikio ya kibiashara.

Hivyo waliiomba SIDO kuongeza zaidi juhudi za kuwafikia walengwa hasa
walio katika maeneo ya vijijini ambako kunawafanyabiashara wengi wenye ndoto za
kumiliki viwanda.

Share.

About Author

Leave A Reply