Thursday, August 22

RAIS WA NAMIBIA AMESEMA KILIMO KINA UWEZO MKUBWA SANA WA KUBADILISHA UCHUMI WETU WAAFRIKA.

0


WINDHOEK. Imekuwa ni tofauti na viongozi wengine wa nchi duniani kujishughulisha na kilimo wawapo na uongozi mkubwa katika nchi. Rais wa Namibia Hage Geingob, licha ya kuwa na ratiba yake kama kiongozi mkuu wa nchi hiyo, hupata muda wa kutembelea mashamba yake.

Hivi majuzi Rais Geingob alituma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha jinsi anavyotumia muda wake mwingine kuangalia maendeleo ya mashamba yake ya mahindi yaliyopo huko Hadaloha nchini humo.

Juzi Machi 21 ilikuwa ni siku muhimu na nzuri nchini Namibia,baada ya mvua kunyesha, aliamua kutembelea katika shamba lake lililopo huko Hadaloha, akiwa katika maadhimisho ya sherehe za 28 za sikukuu ya uhuru wa taifa lililopata uhuru wake mwaka 1990.

Alitoa ujumbe mkubwa kwa nchi za Afrika hasa kusini juu ya nini kifanyike katika kujikomboa kiuchumi.

“Usalama wa chakula ni suala muhimu katika kuondoa umasikini. Kilimo kina uwezo wa kubadilisha uchumi wetu,” aliandika hivyo katika akaunti yake ya Twitter yake akiambatanisha na picha nne zilizoonyesha akiwa shambani.

Rais Hage ameingia katika orodha ya marais wengine wawili wa kiafrika ambao wamewahi kushiriki picha wakiwa kwenye mashamba yao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Muhammadu Buhari wa Nigeria sio tu kwamba wamewahi kuwa wanajeshi hapo zamani bali wawili hao ni wakulima na wafugaji wa ng’ombe.

Viongozi wengine wa Afrika wanaojulikana kwa kufanya shughuli za kilimo ni Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete, Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.

Mwaka jana Kikwete alisema anayo furaha nje ya ikulu ambapo hujishughulisha na kilimo, Jammeh alionekana katika mitandap akiwa akifanya kazi kwenye shamba lake la huko Gine Equatorial wakati mwingine na Bi.Johnson Sirleaf siku za hivi karibuni alisema kilimo ni kitu ambacho alikuwa amepanga kufanya mara baada ya kustaafu urais.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.