Wednesday, August 21

POLISI YAELEZEA JINSI DEREVA ALIVYOMUUZA OFISA UBALOZI SYRIA KWA MAJAMBAZI

0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limeelezea jinsi dereva wa Ofisa Ubalozi wa Syria nchini, Hassan Alfaouri alivyoshirikiana na watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi kumvamia na kumpora  kiasi cha Euro 93,000.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Kamanda Jumanne Murilo amesema Ofisa huyo ambaye ni mhasibu wa Ubalozi wa Syria alikumbwa na mkasa huo Machi 19, 2018, ambapo dereva alibadilisha njia kwa makusudi wakati wakielekea benki kuzihifadhi fedha hizo.

Ameeleza kuwa, baada ya kubadili njia, Alfaouri alimuuliza dereva huyo sababu ya kubadili njia na kutembea kwa mwendo wa polepole, dereva huyo hakujibu kisha alizima gari na kwamba baada ya dakika mbili walitokea watu watatu na kuanza kumjeruhi ofisa huyo kichwani kwa kutumia nondo, na kufanikiwa kumpora fedha hizo.

Kamanda Murilo amesema baada ya majambazi hao kumpora fedha Alfaouri, walitoroka pamoja na dereva huku wakiwa na gari la Ubalozi ambalo walienda kulitelekeza katika bonde la mpunga la Msasani.

RPC Murilo amesema upelelezi unaendelea wa tukio hilo unaendelea na kwamba Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa kushirikana na idara za polisi litahakikisha wahalifu wote waliokula njama wanakamatwa na hatua za kisheria zinachukuliwa.

Aidha, Kamanda Murilo ameyataka mashirika ya umma na yasiyo ya umma kuwa makini yanapoajiri watumishi ikiwemo kuwashirikisha polisi ili kujua wanayetaka kumuajiri kama hana historia ya uhalifu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.