Monday, August 19

OOH DIAMOND! WCB YAPATA PIGO ZITO!

0


Dar es Salaam. Ikiwa ni kama dalili inayooneshwa bundi bado hajaondoka mtaani kwa kundi la Wasafi wa WCB, kundi ambalo liko chini ya msanii anayetamba kwa kuwapagawisha mashabiki wake awapo stejini, Simba Diamond Platinumz, msanii huyo leo amepata pigo zito baada ya kukimbiwa na mpiga picha wake wa siku nyingi Andrew ‘Kifesi’.

Kifesi anamkimbia Diamond Platinumz ikiwa ni miezi michache tu tangu mwanamuziki huyo akimbiwe na mzazi mwenzake raia wa Uganda, Zarinah Hassan, maarufu kama Zari the Boss Lady, kufuatia kashfa nzito ya Diamond kuchepuka na mwanadada mwenye nyonga laini Hamisa Mobeto, na kufanikiwa kuzaa nae mtoto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mpiga picha Kifes, ameandika ujumbe unaoelezea yeye kung’atuka kunako nafasi yake ya upigaji picha, ambapo ameamua kujipangia kazi nyingine tofauti na aliyokuwa akiifanya kwa boss wake Diamond.

Kifesi

“Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku niloamua kufanya uamuzi yatagobadili maisha yangu, nimeamua rasmi kuacha kazi kama Mpiga picha wa Diamond na mwajiriwa wa WCB. Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kaz kwa mtu alokua zaid ya Rafiki kwangu naacha kaz ambayo ni ndoto ya Vijana wengi out there but to me..i see miaka yangu 4/5 ya kufanya kazi hapa inatosha nimeamua kufuata moyo wangu.” ameandika Kifesi.

Kifesi ameendelea na kutanabaisha umma wa watanzania kuwa, mpango wake wa kumkimbia Diamond, ni wa muda kitambo, kwani amekuwa na wazo hilo kwa muda wa mwaka sasa.

“Ni uamuzi nilokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivo kwa waajiriwa wengi is so hard kufanya uamuzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE NEED TO MAKE CHANGE. Naacha kazi to persue my Dreams life ikiwamo Kujiajiri. Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence.  reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu.. Naacha hii kaz ili niwe karibu zaid na Mungu wangu kwa iman yngu kama. Aliandika katika ukurasa wake huo” ameongeza Kifesi.

Kifesi amemaliza kwa kuomba msamaha kwa watumishi wote wa WCB endapo kama watachukia uamuzi huo, na endapo kama walikuwa wamekoseana kwa siku alizofanaya kazi Wasafi.

“Tusameheane pale tulipowai koseana we are just humans tuna mapungufu tunakosea..hatutakua pamoja kikaz but  Nina iman tutaendelea kua marafiki. God bless u.. Uzid kufika unapopenda kufika.. GOD Bless me.. God bless my next Hustles #happysabbath Day”, amehitimisha Kifesi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.