Wednesday, August 21

OFISI YA MKOA WA KATAVI YALAUMIWA KWA KUTOKUZINGATIA USAFI.

0


Na Mwanadishi wetu-Katavi.

IKIWA Serikali ya Mkoa
wa Katavi wanahimiza zoezi la Usafi kwa wananchi katika maeneo yao na kuwatoza
faini wasiozingatia zoezi la Usafi,DAR
MPYA
 ameshuhudia kichaka kikubwa cha
nyasi zilizozunguka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kinachomshangaza  ni kuona wananchi wakihimizwa kufanya Usafi
halafu wao wakishindwa kuzingatia zoezi hilo ambalo ni Muhimu kwa kila mmoja na
kila taasisi ya kiserikali na binafsi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi
wa Manispaa ya Mpanda Mkoani humo Alex Kishiwa,Anthony Mwalu,Rosemarry Paulo na
Paulina Sayi kwa upande wao wameitupia lawama ofisi ya Mkoa kushindwa
kutekeleza dhana hiyo ya usafi licha ya kuhumiza ufanyike kwa watu wengine.

Vilevile wamebainisha kuwa  kama kungekuwa na watu wanaotoza faini kwa
wasiozingatia Usafi tofauti na Serikali basi Mkoa nao wangepigwa faini kwa
kutozingatia kufanya Usafi katika eneo lao la kazi.

Aidha waliongeza kuwa agizo la kufanya
usafi lililotolewa na rais wa nchi Dkt John Magufuli ni sheria kwa kila mtu na
kila taasisi ya kiserikali na binafsi 
hivyo Mkoa kupuuza kuzingatia kufanya usafi ni aibu kubwa kwa serikali
hiyo ya mkoa.

Sambamba na hayo walishauri wahusika kufanya Usafi maana hapa mnahatarisha maisha ya watu kama ikitokea mtu akachoma moto basi utaleta madhara kwa watu.


Share.

About Author

Leave A Reply