Friday, May 24

OFISI YA CHADEMA MKOA WA KATAVI YA VAMIWA.

0


Na George Mwigulu,Katavi.

Ofisi Kuu ya
Mkoa wa Katavi ya  Chama Cha Demokrasia
na  Maendeleo (CHADEMA) imevamiwa na watu
wasiojulikana na kupora baadhi ya nyaraka muhimu za chama hicho ikiwa pamoja na
vifaa vya samani ya zaidi ya laki nne na ishirini elfu.

Akitoa taarifa
hiyo jana Katibu wa  Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA )Mkoa wa Katavi Almasi Ntije aliiambia MAIIRA  kuwa mnamo wa saa tatu asubuhi alipokea
taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa Katibu wa Umoja wa vijana wa chama cha
demokrasi na maendeleo (BAVICHA)  jimbo
la Mpanda Mkoani humo  Maulidi Maulidi
aliye kuwa amekwenda  kufanya usafi.

Ntije alisema
kuwa Maulidi  baada ya kufika na  kuugusa mlango wa ofisi hiyo  ulifunguka kwa urahisi na baada ya kuingia
ndani alikuta baadhi ya mafaili ya nyaraka zimetupwa chini na kusabalatishwa
hovyo huku zaidi ya viti kumi nane  na
luniga  vikiwa havione mahala vilipo.

Aidha alisema
kuwa nyaraka zilizoibiwa ni nyaraka za uchaguzi unaoendelea ndani ya chama  wa Chadema msingi ngazi za vitongoji
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye faili la Mkutano Mkuu Kamati tendaji
Sekretariet za Wilaya na Mkoa

Katibu huyo
alisema kuwa kitendo hicho ni cha kiharifu kama uharifu mwingine unaotokea
licha ya tukio hilo pia kulihusisha na 
tofauti za  kiitikadi za siasa
kwani wamekuwa wakishuhudia baadhi ya watu wasiowafahamu  wakifika ofisini hapo.

‘Ndugu waadishi
kitendo cha kuvamiwa na kuvunjwa ofisi yetu ya Mkoa…ni  mfululizo wa matukio mengine ambayo yamekuwa
yakitokea mahali tofauti tofauti nchini mwetu.Tayari tumeshatoa taarifa kwa
mamlaka ya jeshi la polisi wilaya ya Mpanda hivyo tunaimani wahalifu hao
watatafutwa popote walipo na kufikishwa mbele ya sheria’Alisema.

Naye Kamada wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Damasi Nyanda baada ya kutafutwa alisema kuwa
hajapata taarifa zozote za kuhusiana na tukio hilo hivyo kuahidi kulifuatilia.

Kwa upande wa
baadhi ya  Wanachama wa cha hicho Malunde
Kija,Maulid Maulid,Wande Rashidi na Pili Mohammed kwa nyakati tofauti walisema
kuwa kitendo cha kuvamiwa ofisi ya chama           Mkoa
ni hakikubaliki,Hivyo wanaliomba Jeshi la Polisi kuwatafuta waharifu hao na
kuwachukulia hatua kali dhidi yao.

MWISHO.

Share.

About Author

Leave A Reply