Monday, August 19

NONDO AWASILI DAR, ASEMA HAJAPATA BARUA YA KUSIMAMISHWA CHUO

0


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini-TSNP, Abdul, amefunguka kuhusu kusimamishwa chuo, ambapo amesema hajapata barua ya kusimamishwa masomo yake hadi pale kesi inayomkabili ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa itakapomalizika.

Nondo amesema hayo leo wakati akzungumza na wanahabari baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Iringa.

“Barua ya kusimamishwa chuo naiona mtandaoni, sina simu sina mawasiliano yoyote,kuna mtu alikuwa ananionyesha nikawa naiona, nikapata taarifa kwamba hiyo taarifa ni yenyewe,” amesema.

Aidha, Nondo amewashukuru Watanzania na taasisi za watetezi wa haki za binadamu ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu-LHRC kwa kupambana hadi anapata dhamana mahakamani.

“Nashukuru ndugu zangu nashukuru taasisi za LHRC, sababu wenyewe wamekuwa wakipambana kujua kipi kimeendelea kuhusu mimi, nashukuru TSNP, watanzania wote walioko ndani na nje kwa sababu pia wenyewe walikuwa wakitaka kufahamu niko wapi naendeleaje,”

Hivi karibuni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anaposoma Nondo, Profesa William Anangisye alisema amemsimamisha masom hadi kesi yake ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa itakapomalizika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.