Saturday, August 24

MEDDIE KAGERE AVUNJA REKODI YA OKWI TPL

0


Mabao mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC yamemfanya mshambuliaji huyo kuvunja rekodi ya ufungaji iliyowekwa na Emmanuel Okwi msimu uliopita.

Mnyarwanda huyo amefikisha mabao 22 mpaka sasa akiwa ndiye kinara katika orodha ya wafungaji mabao mawili zaidi ya Okwi aliyefunga msimu uliopita.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 88 akibakisha pointi mbili ili kutawazwa tena mabingwa wa ligi kuu msimu huu kwa mara ya pili mfululizo. Kama Simba itaibuka na ushindi katika mchezo wao wa Jumanne dhidi ya Singida United katika uwanja wa Namfua watatazwa rasmi mabingwa wa TPL 2018/19.

Kagere aliifungia bao la kwanza dakika ya tano akimalizia pasi ya John Bocco kabla ya kuongeza la pili dakika sita baadae kwa kazi nzuri iloyofanywa na Clatous Chama.

Baada ya mabao hayo ya mapema Simba iliendelea kumiliki mpira lakini walipunguza kasi ya mashambulizi huku wakirudisha pasi nyuma mara kadhaa.

Ndanda imebaki nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 47 baada ya kushuka dimbani mara 36.


Share.

About Author

Leave A Reply