Wednesday, August 21

Maugo yuko fiti kuzidunda na Mtaliano

0


Na saboso jr

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, amesema kwa sasa yupo fiti kupanda ulingoni ili kumchakaza mpinzani raia wa Italia katika raundi ya pili.

 Pambano hilo lisilo la ubingwa litakuwa la raundi 10, katika uzani wa Super middle kg 76 na litafanyika Julai mwaka huu, nchini Italia.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Maugo, alisema anaendelea kujiandaa kuhakikisha anamaliza pambano hilo mapema.

“Nimejiandaa na nipo fiti sina wasiwasi wowote, kikubwa ni maombi ya Watanzania kuelekea katika pambano hilo, nimefanya maandalizi ya kutoka na ninajiamini nitashinda,” alisema.

: Credit:Dimba


Share.

About Author

Leave A Reply