Friday, August 23

MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO WATENDAJI WA MAFUTA WANAOMUUNGA MKONO RAIS SALVA KIIR

0


Marekani imewawekea vikwazo watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini wanaodaiwa kuwa vyanzo muhimu cha fedha kwa Salva Kiir, hatua ambayo inalenga kuongeza shinikizo kwa rais huyo kumaliza mgogoro na mzozo wa kibinadamu nchini kwake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters makampuni na taasisi za serikali huenda katika siku za karibuni zikahitaji leseni maalum ya kufanya biashara nchini Marekani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Inadaiwa kuwa, Serikali ya Sudan Kusini na maafisa ambao ni wala rushwa, wanatumia mapato ya mafuta kununua silaha na kufadhili wanamgambo ambao wanadumaza amani, usalama na uthabiti nchini Sudan Kusini.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema. Makundi yaliyo kwenye orodha yalihusika na harakati ambazo ni kinyume na sera za mambo ya nje na maslahi ya Marekani, kwa mujibu wa waraka uliochapishwa na wizara ya biashara ya Marekani Jumatano.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.