Thursday, August 22

KESI YA NONDO DHIDI YA IGP, AG NA DCI KUSIKILIZWA APRILI 4

0


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itaanza kusikiliza maombi ya Jinai Na. 49/2018 yaliyofunguliwa mahakamani hapo na watetezi wa haki za binadamu dhidi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Katika maombi hayo, Watetezi hao wanaiomba mahakama itoe amri ya kuachiwa huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini-TSNP, Abdul Nondo anayeshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa.

Jaji anayesikiliza maombi hayo, Jaji Rehema Sameji ameitaka Jamhuri kujibu maombi Machi 26 na upande wa waleta maombi kuleta maombi yao ya ziada Machi 27 mwaka huu, na kwamba mahakama itasikiliza hoja za pande zote mbili Aprili 4 mwaka huu.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa maombi hayo, Wakili upande wa waleta maombi, Wakili Msomi, Jebra Kambole amesema Aprili 4, 2018 Mahakama itasikiliza maombi yao ikiwemo mteja wao, ambaye ni Abdul Nondo kupata dhama, kupata haki ya uwakilishi pamoja na kuangalia kama kushikiliwa kwake na Polisi kulikuwa kwa mujibu wa sheria au lah.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.