Monday, August 26

Kalidou Koulibaly beki bora Serie A kwa msimu wa 2018-19.

0


Beki wa kimataifa wa Senegali na klabu ya Napoli ya Italia, Kalidou Koulibaly amechaguliwa kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu ya Italia Serie A kwa msimu wa 2018-19.

Wachezaji wengine walioshinda tuzo za Serie A ni Samir Handanovic wa Inter Milan ameshida tuzo ya golikipa bora wa msimu, Kiungo wa Lazio, Milinkovic Savic yeye amechaguliwa kuwa kiungo bora wa msimu.

Wengine ni mshambuliaji wa Fabio Quagliarella yeye ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa msimu, Nicolo Zaniola wa As Roma yeye ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa msimu.

Huu tunaweza kuuita mwaka wa Africa barani ulaya kwani msimu huu umekuwa wenye manufaa sana kwetu huku tukiwashudia nyota wa Misri Mohammed Salah, Sadio Mane toka Senegal na Pierre Aubameyang toka Gabon wakitwaa viatu vya dhahabu kwa kuibuka wafungaji bora ligi kuu nchini Uingereza EPL huku wakifunga magoli 22 kwa kila mmoja.


Share.

About Author

Leave A Reply