Thursday, August 22

KAGERE AJIWEKEA REKODI AFRIKA

0


Kagere, raia wa Rwanda, ndiye kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara ambayo msimu huu ulimalizika hapo jana  Jumanne, huku Simba ikiwa bingwa.

STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere, mpaka sasa ameweka rekodi ya kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi zaidi msimu huu katika ligi za barani Afrika akiwa nayo 23.

Kwenye ligi kuu mbalimbali barani Afrika, hakuna mchezaji ambaye ameweza kufikisha idadi hiyo ya mabao ambayo amefunga Kagere hadi sasa kiasi kinachompa nafasi Mnyarwanda huyo kuweka rekodi hiyo ya mabao Afrika.

Washambuliaji wafuatao katika ligi mbalimbali Afrika wamezidiwa mabao na Kagere; Ligi Kuu ya Kenya, kinara ni Allan Wanga anayecheza Kakamega Homeboyz, amefunga mabao 18, Mouhcine Iajour wa Raja Casablanca ndiye kinara wa Ligi Kuu Morocco akifunga mabao 18.

Straika Mwape Musonda wa Black Leopards ndiye aliyemaliza kinara wa Ligi Kuu Afrika Kusini akifunga mabao 16, Zakaria Naidji ndiye kinara wa Ligi Kuu ya Algeria akifunga mabao 19. Naidji anacheza Paradou AC.

Ulimwengu Jules wa Rayon Sport ndiye aliyemaliza kinara wa Ligi Kuu Rwanda akifunga mabao 19 wakati Juma Balinya wa Police ya Uganda akimaliza kinara wa ufungaji Ligi Kuu ya Uganda akifunga mabao 19.

Ligi Kuu Misri kinara wa mabao ni Mahmoud Alaa El- Din wa El Zamalek aliyefunga mabao 14, wakati Tunisia kinara ni Taha Yassine Khenissi wa Esperance mwenye mabao 10.


Share.

About Author

Leave A Reply