Wednesday, August 21

HUSSEIN BASHE:UONGOZI NI UTUMISHI NASI TUMETIMIZA HILO KWA WATU WETU.

0


NZEGA. Mbunge wa jimbo la Nzega mjini mkoani Tabora mheshimiwa Hussein Bashe (CCM) amesaidia uboreshaji na upatikanaji wa huduma bora za afya ikiwa katika hatua ya kupunguza changamoto hiyo kwa watanzania jimboni kwake.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi na upanuzi wa kituo cha afya cha Zogolo kilichopo wilayani hapo ambacho kimepandishwa hadhi na kuwa na Hadhi ya Hospitali,amesema ilikuwa ndoto yake kufanikisha tangia kipindi anaomba ridhaa kwa wananchi.

“Hii ilikuwa ni ndoto yangu mwaka 2015 wakati wa kampeni kuhakikisha kituo cha afya cha Zogolo kinakuwa na hadhi ya hospitali kubwa na ya kisasa ili kuweza kuhudumia wananchi wengi ndani ya jimbo la Nzega Mjini.” Alisema mhe,Bashe

Aidha,Bashe amewashukuru wananchi wa jimbo lake,serikali kuu pamoja na watalaam wa halmashauri ya mji wa Nzega na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

“Maendeleo ya watu ni kugusa maisha ya watu, na moja ya njia hizo ni kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii,mathalani upatikanaji wa huduma bora za afya,

“Rais Magufuli amelifanya hili kwa vitendo hapa Nzega kupitia ujenzi na ukarabati mkubwa wa upanuzi wa kituo hiki cha afya cha Zogolo na sasa kuwa na hadhi ya hospitali ya kisasa na ya kuigwa kupitia usimamizi mzuri wa fedha ili kufikia malengo na leo hii tumepokea viongozi wengi wakija kujifunza kwetu namna tulivyofanikisha ndoto hii.” alishukuru mhe,Bashe.

Mheshimiwa Bashe amesema kupitia mradi huo jimbo hilo limefanikiwa kujenga OPD ya kisasa,majengo ya upasuaji,majengo ya wagonjwa mahututi,jengo kubwa la mochwari ya kisasa,maabara ya kisasa,wodi kubwa ya kisasa ya akina mama na watoto pamoja na nyumba za kisasa za watumishi wa hospitali.

“Niliomba serikali kuu fedha na ikanipatia huku katika awamu ya kwanza jumla ya Shilingi Milioni 500 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi na kuboresha miundombinu katika kituo hiki cha Afya ili kiwe na hadhi ya Hospitali,

“Na sasa tunategemea awamu ya pili kupata jumla ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba zikiwemo X-ray na Ultra-Sound machine panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu.” Aliongeza Mhe Bashe.

Akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa Nzega mjini kwa niaba yao ametoa shukrani za dhati kwa viongozi wote ambao walijitoa katika kuhakikisha wananchi wa wilaya Hiyo wanafanikiwa kupata hospitali ambayo itasaidia uboreshaji wa huduma za afya jimboni hapo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.