Friday, August 23

FELIX TSHISEKEDI KUWANIA URAIS DRC.

0


Kinshasa. Mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa Kongo DRC, Felix Tshisekedi, amechaguliwa kuwania urais wa nchi hiyo, na muungano wa upinzani UDPS, katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo uliopangwa kufanyika baadae mwaka huu.

Felix amechaguliwa siku ya leo Machi 31, 2018 mara baaada ya kukamilika kwa mkutano wa wajumbe wa UDPS, mkutano ambao umefanyika katika mji mkuu wa Kinshasa.

Mara baada ya kuchaguliwa, Felix alipata wasaa wa kuzungumza, na ndipo aliposema ana matumaini ya kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Nina imani kwamba UDPS itaingia madarakani mwaka huu kuweka mambo sawa nchini” amesema Felix.

Felix amechaguliwa baada ya kupata kura 790 kati ya 803 za wajumbe wa chama hicho, na sasa anachosubiri ni kufika kwa tarehe za uchaguzi ambao umepangwa kufanyika tarehe 23 Disemba 2018, baada ya kuahirishwa mara mbili, jambo lililosababisha ghasia zilizohofiwa kuliingiza taifa hilo vitani.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.