Saturday, August 24

DC MPANDA WAJASIRIAMALI WASIO NA VITAMBULISHO KUFUNGIWA BIASHARA

0


Na George Mwigulu,Katavi.

MKUU  wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian
Matinga amewataka wajasiliamali wote wasio na vitambulisho vya Ujasiriamali
kuhakikisha mara moja wanakuwanavyo si vinginevyo hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao ikiwa sanjali na kuzuiwa kuendelea kufanya biashara.

Tamko hilo
amelitoa jana ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya uwasilishaji fedha za
vitambulisho vya ujasiriamali kwa waadishi wa habari ya kuanzia Januari 12,2019
hadi Mei 17,2019,Ambapo jumla ya vitambulisho 2,311 sawa na vitambulisho 1,308 kutoka
Manispaa ya Mpanda na 1003 vikitolewa Halmashauri ya Nsimbo.

Lilian
alifafanua kuwa jumla ya Tsh 46,220,000/=katika Wilaya ya Mpanda  zimekusanywa ikiwa fedha hizo ni sawa na
vitambulisho  vya ujasiriamali  2,311 vimenunuliwa.

Hivyo alibainisha
idadi hiyo  ni ndogo sana ukilinganisha
na vitambulisho vya ujasiriamali 25,000 walivyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi aliyeondoka madarakani Amosi Makalla .kwa sababu hiyo alisema inawapasa
kujielekeza kwa nguvu kuhakikisha vitambulisho hivyo vinanunuliwa.

Mkuu wa Wilaya
huyo aliongeza kuwa tayari alishatoa muda wa kutosha kwa kila mjasiriamali kuwa
na kitambulisho  ifikapo Mei15,2019  ambapo  muda huo umekwishapita kwa mjasiriamali asiye
na kitambulisho kuwa nacho ikiwa kwa sasa watafanya opareshini maalumu
kuwabaini wajasiriamali wote wasio na vitambulisho.

 “Hatuwezi kuwavumilia tena wajasiriamali wasio
na vitambulisho vilivyotolewa na rais John Magufuli  vyenye  lengo la kuwaepusha na adha ya tozo za kila
siku za tsh 300 hadi tsh 500  kwa
wajasiriamali wenye vipato kisichozidi tsh 4,000,000/=kwa mwaka …ni jukumu la
kila mjasiriamali kuwa na kitambulisho kinyume na hapo ni afadhari kusitisha
kufanya biashara hadi pale atakuwa nacho”Alisema

Aidha alizidi
kutoa  rai kwa wajasiriamali kuwa na moyo
wa uzalendo kununua vitambulisho hivyo vinavyouzwa tsh20,000/- kwani kufanya
hivyo ni sawa na kuchangia kodi kwa taifa lao. fedha ambazo zitatumika
kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa iliyoibuliwa na serikali.

Nao baadhi ya
Wajasiriamali wa soko la Kilimahewa lililopo  Manisapaa ya Mpanda Esther Kasanda,Maria John
na mwenyekiti wa soko hilo Filbert Musa walisema kuwa kitendo cha kufunga
biashara zao kutokana kutokuwa na vitambulisho ni  kibayamaana kina lengo la kuwafanya ombaomba.

Vilevile
waliiambia  Serikali ya Manispaa ya
Mpanda kuwa madhara makubwa yatatokea pindi biashara zao zitakapo fungwa kwani
watengemea wimbi kubwa la kuongezeka kw a waharifu ambao kipato chao
kilitengemea biashara ndogondogo.

Hivyo waliiomba
serikali kuzidi kuwa wavumilivu maana wanania kubwa ya kununua vitambulisho
hivyo licha ya kuchelewa kwa baadhi yao kwani hali yao ni ngumu sana kifedha
hasa katika kipindi hiki.

Share.

About Author

Leave A Reply