Tuesday, March 19

DC GODFREY NGUPULA “HAKUNA MVUTANO HALISI KATI YA MEMBE NA DKT BASHIRU

0


Tabora

Mkuu wa wilaya ya Nzega na mjumbe wa kamati ya Siasa ya wilaya hiyo Mheshimiwa Godfrey Ngupula amesema kuwa kwa siku kadhaa sasa kila kona ni habari ya mvutano kati ya Membe na Dkt. Bashiru.

Na haswa mvutano huu unavyoongezwa chumvi na pilipili katika magazeti na mitandao ya kijamii.

Nilikuwepo Nzega wakati Dr. Bashiru anatoa ufafanuzi wa kilichotokea,namnukuu “Mimi kwanza nilipoyatamka yale Geita katika maongezi yangu wala sikuwa namaanisha kumuita Membe, utaratibu wa kuitana kichama naujua na unajulikana.

“ikitaka kumuita basi nitafanya hivyo kwa barua au kwa simu lakini, nilisema nahitaji kukutana na Membe ofisini kwangu, tena wala sio kwa mashtaka au tuhuma, bali aje tuongee tuongezane ujuzi juu ya kulisukuma gurudumu hili la maendeleo.”

“Hakuna popote nilipowahi kumuhusisha Membe na Musiba.

Musiba anayasema anayoyasema kama mwanaharakati, Kuzingatia anachokisema au kumpuuza ni hiari ya mtu,kwa hiyo ni kweli Membe namuhitaji, na nishukuru ameafiki kuja.

Lengo langu ni zuri tu, tuongee tuimarishe chama na tuijenge nchi.”

“Ndugu zangu wanachama, kazi kubwa tumeshaimaliza. Tunaelekea kwenye uchaguzi,mambo ya kutugawa ni mengi, lkn tuwe makini na twendeni tukapiganie umoja na mshikamano wa chama chetu.”

“Lakini, tukiwa wakweli katika ubinadamu mara nyingi taarifa kutoka sehemu moja kwenda nyingine inaweza kupotoshwa kwa malengo mahususi. Ni rai yangu kwa wanachama wenzangu, tusonge mbele na chama chetu.
Hakuna mvutano wowote halisia kati ya Membe na Dr Bashiru. Nimemsikia mwenyewe katibu mkuu wetu akitolea ufafanuzi alipokuwapo Nzega. Adui anahitaji sana kupata mlango wa kuingilia atusambaratishe. Tushtukie mapema na tuzibe mwanya huo.”amesema Ngupila.

Share.

About Author

Leave A Reply