Thursday, August 22

Cardiff,Middlesbrough FC zawania saini ya Samatta

0


BAADA ya kuifanikisha timu yake ya Genk kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), ofa zimeanza kumiminika kwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta.

Licha ya kwamba zimebakia mechi mbili ligi hiyo kufikia tamati lakini kikosi hicho cha KRC Genk, kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, kimetangazwa kuwa mabingwa kwa kufikisha pointi 51 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Mbali na kuisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa na Ligi ya Ubelgiji, Samatta, ameibuka kuwa mfungaji bora akipachika jumla ya mabao 23 kitu kinachozifanya timu kwamba Ulaya kuanza kutuma maombi ya kutaka kumsajili.

Tayari timu mbili kutoka nchini England zinadaiwa kuitaka saini ya Mtanzania huyo ambazo ni Cardiff City iliyoshika nafasi ya tatu kutoka mwisho Ligi Kuu nchini humo pamoja na Middlesbrough FC.

Hii si mara ya kwanza Samatta kupata ofa mbalimbali kwani timu nyingine zilizowahi kuhusishwa na Mtanzania huyo ni Everton, West Ham zote za England na kule Ujerumani zikiwepo baadhi.

Kwa upande wao Cardiff City hii ni mara ya pili wanarusha ndoano kwa Samatta kwani walianza kufanya hivyo Januari mwaka huu wakitenga donge nono lakini Genk wakalitupilia mbali.

Samatta ameifungia Genk mabao 62 katika mechi 155 za mashindano yote tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika ligi ya Ubelgiji pekee amefunga mabao 47 katika mechi 122, kwenye Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa na Europa League amefunga mabao 14 katika mechi 24.


Share.

About Author

Leave A Reply