Saturday, August 24

BREAKING NEWS: SIMBA MABINGWA LIGI KUU TANZANIA BARA 2018/19

0


Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamenyakua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kuichapa Singida United mabao 2-0 kwenye uwanja wa Namfua Singida.

Kwenye ushindi huo magoli ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere dakika ya 10, na John Bocco 60.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu, ikiwa bado ina michezo miwili mkononi.

Huu ni ubingwa wa pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita 2017/18 ikiwa njiani kuelekea Singida, na ni ubingwa wake wa 19 kwenye ligi hiyo, nyuma ya mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao wameshachukua ubingwa huo mara 26.

Ubingwa wa Simba umepatikana katika miaka ya 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012, 2018 na 2019.


Share.

About Author

Leave A Reply