Thursday, August 22

YAANI WASOMI SIWAELEWAGI KWA KWELI

0
Yaani mi wasomi siwaelewagi kiukweli, labda sababu sikusoma sana  lakini nawaangaliaga halafu na jichekea kimoyomoyo. Yaani utaona wanajifanya wanajua kumbe ukiangalia kwa makini, utajua kumbe jamaa hawajui mambo mengi sana. Lakini lazima kuwaonea huruma, unajua wao wakati wako shule walikuwa wako bizi na vitabu wanajitahidi kukesha kwa kuweka miguu kwenye ndoo za maji baridi ili wasipate usingizi wakeshe wanasoma. Mchana wanasoma, usiku wanasoma, hawajui Yanga wala Lipuli wala Asno, wao ni kusoma tu, hata kucheka wanaona kma wanapoteza muda wa kusoma, na kweli  wanaenda vyuo vya juu na huko wanasoma zaidi, wanaenda Ulaya kule tena wanaendelea kusoma, mambo yanayoendelea duniani wao yanawapita. Wakimaliza shule wanajua kweli mambo waliyosomea, utasikia huyo profesa wa miti, au dokta wa udongo, wanajua kila kitu kuhusu taaluma yao, lakini ukiwaambia hebu cheza singeli wanacheza kama wazungu, hawajui starehe ya kucheza kiduku, wala rumba.  Ukiwauliza kama wanamjua Juma Necha au Feruzi wanakuangalia tu.  Sasa ngoma inakuja hawa jamaa si ndio wanachaguliwa kuwa viongozi wa nchi, wao wanajua mambo ni kuwa bizi tu, wanaendeleza mambo yao yale ya kukesha kwenye ndoo hata kwenye maisha. Halafu wanadhani watu wote wanatakiwa waishi kama wao, ukimwambia twende mpirani hataki, twende dansi, ndio kabisa hataki, labda umwambie twende maktaba kusoma vitabu hapo ndipo anakuona wewe wa maana.  Hawa hawa wasomi utasikia, ‘Nilisoma Ulaya mambo ya uchumi, wazungu wanasema  lazima kila mtu alipe kodi ili nchi iendelee’, Sasa sie wengine huwa tunaenda kunywa bia saaana ili kusaidia kodi ipatikane, hapo ndipo utamshangaa msomi, anakuja tena anatunga sheria za kukataza usinywe bia, eti nenda kafanye kazi ulipe kodi, jamani hivi usomi wote huwa hawaoni kuwa wanywa bia tunalipa sana kodi bila kushurutishwa? Yaani wakipata tu uongozi wanaanza kuweka sheria za kupunguza muda wa kunywa, sijui hivi hawaoni kuwa wanapunguza muda wa kulipa kodi. Unajua mie huwaga siwaelewi hawa jamaa, siwaelewi kabisaaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.