Tuesday, August 20

MUHIMU KUCHEKA , ukishindwa jitekenye na vichwa hivi vya habari

0


 Aise nyie kazi yenu si kufungana magoli? Sasa hii ishu ya kupigana mikono inatokea wapi? Acheni hizo, mwisho tutasikia mnapiga wenzenu vichwa

 Kiukweli imelazimika wafanyakazi wote fekifeki wa blogu hii tuitwe kwenye kikao feki tuangalie kichwa hiki cha habari na kukidiskas. Baada ya kikao maazimio yanasema 
i.  Maziwa hapa ni yale ya ng’ombe au mbuzi kwa kizungu milk….swali nani anachea maziwa yetu, kumbe tunakunywa maziwa yaliyochezewa machezo mchafu?
ii. Maziwa hapa maana ni yale kwa kizungu yanaitwa lakes. kama Lake Nyasa, Lake Victoria na kadhalika…swali je ni kitu cha ajabu watu kucheza wachafu kwenye maziwa? Kwa kuwa maziwa hayo yamejaa  maji yanayoondoa uchafu basi poa tu, kachezeni mtatakata tu
iii. Mchizi wa ofisi anadai maziwa hapa ni yale ya wamama ambayo watoto wananyonyaga… kiukweli watu wengi wanachezea vibaya haya maziwa aka manyonyo
Sasa serikali imeshtukia mchezo mchafu kwenye maziwa yepi?

 Ok so kimsingi ni mmoja wa wavuta bangi, wengine wanavuta ili walime, wengine ili waondoe woga wa kuwatokea wapenzi, wengine wanavuta ili waimbe vizuri, ila kimsingi wote ni wavuta bangeee

 Simba mkorofi huyu au mbao hiyo ilikuwa feki kama zile za fanicha za Mchina,

 Kwani kubeba unga ni tatizo? Mbona wenzenu  huku kijijini tukitoka mashine kusaga tunabeba tu bila shida, kwanini sasa huyu anyatiwe? Nyie watu wa mjini bwana  mna mambo, kumbebesha mtu unga tu imekuwa nongwa

 Sijaelewa kazaa nae au hakuzaa nae? Yaani kashinda kitu gani?

 Ukiona umeweza kumfuga simba ujue huyo ni paka mkubwa tu sio simba. Weee ufuge simba kwa uchawi gani?

 Hahahaha jamani woga gani tena, Mange aandamane ndio polisi watishike? Si wamuache tu aandamane, kwanza yuko Marikani so whats problem. Nyerere aliwaambiaga watu waliokuwa wakimbebza Mrema  kuwa waachiwe hata maiti huwa inabebwa…..

Halooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo, mmesema nini nyie???????????Read More

Share.

About Author

Comments are closed.