Wednesday, August 21

MADREVA KARIBUNI DAR LAKINI ACHENI KUPANIKI OHOOO

0
Oyaa leo ishu inahusu madreva, sio wote bali wale wanaotaka kuja Daslam. Leo nimeona nifanye jambo zuri la kutoa elimu kwa madreva wanaotaka kuja Daslam. Mnajua zamani kabla Dodoma haijapanda cheo, sehemu yoyote nje ya Daslam kulikuwa kunaitwa mikoani, sasa siku hizi kibao kinageuka  nje ya Dom ndio mikoani, jiji hili moto nalo eti linaanza kuitwa mkoani?  dahhh kweli hujafa hujaumbika. Okee ishu ni madreva nisije nikasahau mada. Ndugu zangu madreva mnaetaka kuja Daslam, taarifa hii iwafikie ili mkiyakuta ya huku msipaniki. Unajua kuna wale ndugu zangu wa kuleee, wakipaniki kidogo tu wanajinyonga, kuna wengine wa kuleee wakipaniki hawachelewi kuchukua mapanga, wengine wa kuleee wakipaniki wanapandisha mori, hapo ujue sime inahusika, sasa chonde chonde wajameni pateni elimu ya bure leo ili mkija msije kujikuta mnapaniki kila kona.
Sheria ya huku ni moja tu, kila gari ni mkweche. Haijalishi kama ndio kwanza linatoka shoorum au umetumia miezi mitatu au umeagiza wiki mbili tu toka Ujapani, kikubwa sheria iko moja tu, kila gari ni mkweche. Kwa wale ambao hawajui maana ya mkweche ni kuwa kila gari ni bovu. Hii ndio sheria ya hapa Daslam, wenyewe tumeshazoea, ukisimamishwa tu na walinzi wa barabara unaanza kuomba msamaha kwa kuwa na gari bovu. Yaani usianze kujidai unashangaa kwanini umesimamishwa au uanze kujitetea kuwa gari lako jipya, aise hiyo itakuwa kosa la ziada. Unajua hata haya magari mapya hawa jamaa huwa wanagundua ubovu, unaweza kukuta indiketa zinapiga kwa spidi ndogo mno au kubwa mno, au tairi zimekosa upepo wa kutosha, au umezidisha mno upepo, au pengine hata vioo vyako vichafu, we ukiambiwa ‘ Mzee gari lako lina makosa’ usianze mjadala, hawa jamaa hawakupewa mafunzo ya kujadiliana, usije ukajikuta usipopapenda.
Ushauri mwingine ni kuwa huku kwetu bodaboda hawaruhusiwi kufwata sheria. Unashangaa nini? Huo ndio utaratibu wetu, boda boda haruhusiwi kusubiri taa ya kijani , yeye anapita saa yoyote na popote mradi roho yake imtume. Anaruhusiwa kuovateki upande wowote, hivyo usifungue mlango wa gari kabla hujaangalia, ukimgonga au mudhuru bodaboda, ndugu zake hukusanyika kwa wingi kama vile wanavyokusanyika kunguru pale mojawao akiumizwa au kuuwawa.
Naona niishie hapo kama hujanielewa acha gari Chalinze we njoo kwa miguu hapo hakuna shida.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.