Saturday, August 17

KUWA NA MCHEPUKO INAHITAJI AKILI YA ZIADA

0
Unajua kuna mambo mengine huwa tunaongea na kucheka na kutania lakini ni mambo magumu yanayohitaji uvumilivu, sayansi, ubunifu, uwongo na kadhalika kuweza kufanikiwa vizuri. Hivi mnajua hakuna jambo gumu kama kuwa na ndoa halafu kuwa na mchepuko?  Mi nawashangaa sana jamaa ambao wamo katika ndoa kisha wana michepuko, hivi mnawezaje kutimiza masharti magumu ya mchezo huo. Juzi kulikuwa na sikukuu yenu mpendanao, huku mwandani anajua mtakuwa wote siku hiyo na mchepuko anajua mtakuwa wote siku hiyohiyo, sasa hapo ndio najiuliza unatumia mbinu gani? NIlijaribu kuulizia rafiki zangu wawili ambao wamo kwenye mtiti huo majibu yao yameniacha hoi.
Kwanza kuna huyu jamaa yangu ambaye ana mke mzuri tu lakini kajitosa kuwa na mchepuko mkorofi. Kanambia yeye hana tabu na siku ya Valentine kulikuwa hakuna namna ilikuwa lazima atafute njia ya kuwa na mchepuko maana kinyume cha hapo tatizo kubwa lingetokea. Hivyo alianza kumshawishi mkewe kuwa waachane na mambo ya Valentine kwa kuwa kasoma kwenye mtandao kuwa sherehe hizo ni za kishetani. Na mkewe ambaye ni mtu wa dini wakati huo alikuwa kishafanya mipango mingi ya kumtengenezea mumewe chakula cha nguvu kwa ajili ya siku hiyo, ikalazimu akagawe chakula kwa jirani ili asijikute anasherehekea sikukuu ya mashetani, jamaa akaaga anaenda angalia mpira na wenzie klabu, akapata mwanya kwenda kula sikukuu na mchepuko.  Halafu kuna huyu mama jirani tumezoeana naye kanipa stori yake ya Valentine , akanambia alijaribu kila njia kumtoka mumewe aende kwa kibenten wakafurahie Valentine, dili likakwama. Mamaa alimtaarifu Kibenten kuwa sipike wala nini, amsubiri yeye atakuja na chakula toka hoteli moja kali sana mjini. Basi hapo mamaa alianza kumlainisha mumewe kuwa kuna rafiki yake alifiwa na mama yake anataka kwenda kumpa pole, jamaa akakubali na kumwambia mkewe itakuwa vizuri kwa kuwa ni siku ya Valentine wasindikizane itakuwa na uzito zaidi, baada ya dakika kumi, mamaa akaja na stori kuwa safari imekufa maana rafiki yake kumbe kasafiri. Baada ya hapo akaanza kujidai anataka amtengenezee mumewe chakula kitamuu, anataka kwenda Kariakoo kununua viungo vya pilau, jamaa akamwambia mkewe aachane na pilau, leo wale ugali mchicha kama siku ya kwanza walipokutana enzi za ubachela. Mamaa akaona akubali yaishe akamtwangia Benten simu kuwa kapatwa na tumbo la ghafla hivyo haji.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.