Tuesday, August 20

KIFO KINATISHA BWANA WEWE

0
Aise kifo kinatisha. Umeshaona watu wanavyoongea kwa sauti ya chini wakiwa karibu na maiti? Wanasaikolojia wanasema kuwa hii ni kutokana na woga wa kifo. Utaona gari lililobeba maiti linawasha taa kutaarifu kila mtu kuwa kuna kitu si cha kawaida kinakuja, watu wote wanasogea pembeni kwa heshima, nimeshaona watu waliobeba maiti wakizuia gari zisipite mpaka wao wapite wawahi kuzika, wote woga huo. Sasa mkasa kiboko umemkuta jamaa yangu. Baada ya kupata mtoto wa kwanza yeye na mkewe walifurahi sana. Miezi michache baadae walianza kukosa raha baada ya kuhisi kuwa mtoto wao huwa hatoi sauti ya kuonyesha anataka kuongea, mwisho ikawa wazi kuwa wamezaa mtoto bubu. Siku moja ghafla wakasikia mtoto anasema ‘Bibi bibi’, ilikuwa furaha kubwa wazazi wakajua kumbe mtoto wao anaongea. Lakini furaha yao ilikuwa ya muda mfupi, bibi wa mtoto akafariki siku hiyohiyo. Baada ya hapo mtoto akaendelea kuwa bubu. Mwezi baada ya msiba mtoto akaamka anatamka, ‘Mjomba mjomba’, wazazi tena wakalipuka kwa furaha, baada ya muda mfupi furaha yao ikaisha, walipopata habari kuwa kuna msiba wa mjomba wa mtoto. Sasa ukaanza wasiwasi, maana ikaonekana kila mtoto akifungua mdomo na kutaja jina la mtu anafariki. Wakaanza kuona heri abakie bubu. Baada ya miezi sita ya mtoto kuwa bubu siku moja akaamka na kusema ‘Baba baba’, basi kilio kikaanza pale pale wakajua jamaa yangu ndio safari imefika. Jamaa akawa anahaha, hakai wala hasimami, machozi yana mtoka hovyo. Siku nzima ikawa anafanya mambo ya ajabu, kakusanya nguo zake kazikunja kasha kazichoma,  akachoma nyaraka zake nyingi tu, akaanza kugawa vitu vyake muhimu. Mkewe akaomba kuongea nae, mume akagoma na kusema ‘Usinipotezee muda si unajua nina dakika chache tu za kuishi? We niache’. Mke akasisitiza kusikilizwa, hatimae jamaa akakubali  kusikiliza neno la mkewe. Kwa upole Yule mama akamwambia mumewe, ‘Mume wangu samahani kwa ntakalokwambia aomba unisamehe, kiukweli mtoto huyu si wako nilichepuka kidogo na baba yake amefariki masaa mawili yaliyopita’.  Jamaa alipigwa bumbuwazi kwa muda kasha akapiga ukulele wa furaha na kuanza kusema, ‘Asante Mungu asante Mungu’, hapohapo akamkumkumbatia mkewe kwa furaha na kumsifu, ‘Asante mke wangu leo ndio nimejua unanipenda kwa dhati, umeniokoa na kifo mke wangu’ Kifo kinatisha bwanaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.