Sunday, August 25

MFUKO WA MAWASILIANO UCSAF WATUMIA ZAIDI BILIONI 100 KUFIKISHA HUDUMA YA MAWASILIANO NCHINI

0


@Darmpya.com

Dodoma. IMEELEZWA kuwa jumla ya fedha shilingi Bilioni Mia Moja Kumi na nane (118 bil), zimetumika kwa kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wakazi zaidi ya Milioni tano nchi nzima.

Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, ambapo yatarajiwa kuanza kufanyika Aprili 27 na kilele chake kuishia Aprili 30 mwezi huu.

Eng. Ulanga amesema kuwa huduma za mawasiliano zimewafikia watu milioni 5, ambapo ametaja kata 703 zenye vijiji 2501 kuwa wanufaika waliofikiwa na huduma za mawasiliano mkoani Dodoma.

“Tangu kuanzishwa kwa mfuko wa mawasiliano kwa wote, mfuko huu umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa mawasiliano nchini, na wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano,

“Wakati mfuko unaanza takribani asilimia 45 tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu,lakini mpaka sasa takribani asilimia 94 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu”. Ameeleza Mhandisi Ulanga.

Aidha, katika maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma, na mgeni rasmi kuwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Eng. Ulanga amesema kuwa Mfuko wa mawasiliano umeandaa shughuli mbalimbali yakiwemo maonesho ya watoa huduma hizo nchini.

Mbali na hivyo, Kiongozi huyo amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na Shughuli ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilayani Bahi, sambamba na kuzindua clabu za Tehama katika shule za sekondari jijini hapa, pamoja na kugawa kompyuta katika wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Share.

About Author

Leave A Reply