Saturday, August 24

360 news

0


Wasanii wa muziki wa Bongo fleva nchini, Aslay na Nandy wamepigwa faini ya milioni 5 kwa kosa la kuimba wimbo wa Subalkheri bila kibali maalumu kutoka kwa watunzi na wamiliki wa wimbo huo ambao ni kikundi cha Utamaduni cha taarab asilia visiwani Zanzibar.

Kikundi hicho kilikusudia kuwafikisha mahakamani wasanii hao lakini kabla ya kuchukua hatu hiyo kiongozi wa Aslay na Nandy walifika visiwani humo na kufanya mazungumzo na kikundi hicho.
Ambapo viongozi hao walikiri kufanya kosa hilo la kukariri na kuimba wimbo huo bila kibali toka kwa wamiliki hao na kupitia kosa hilo kikundi hiko cha taarabu kimewataka walipwe milioni tano kama adhabu.
Katibu Mkuu wa kikundi cha utamaduni cha tarabu asilia, Taimur Rukuni Twaha, amesema kikundi hicho cha tarab kimewataka wasanii hao kulipa faini kutokana na kuimba wimbo huo bila ya ridhaa.
Twaha amesema licha ya kukiri makosa hayo pia meneja wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho cha tarab kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao nyingine za zamani.
Katibu huyo amesema kuhusu nyimbo zao kuimbwa tena hilo bado hawajaafikiana kwa sababu walishapewa agizo na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dk Salmin Amour Juma wakati akiwa rais, kuwa wasikubali nyimbo zao za tarabu asilia kuzibadili na kuzifanya katika mfumo wa muziki wa kisasa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.